Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

FAHAMU MRADI WA MABASI YAENDAYO KWA KASI UNAOENDELEA KUJENGWA BARABARA YA MOROGORO, DAR ES SALAAM

DSC_0678 Mfano halisi wa jinsi itakavyokuwa barabara ya mabasi yaendayo kasi inayoendelea kujengwa kwenye barabara ya Morogoro, katikati ni sehemu ya kituo cha abiria na mabasi ya kasi, pembeni ni barabara ya magari ya kawaida.

Ufuatao ni ufafanuzi wa namna mradi huo utakavyofanyakazi kama ambavyo picha ya mfano inavyoonesha. Ufafanuzi huu ni kwa mujibu wa mdau wa Blog ya RAHA ZA PWANI (Said Powa)

“Pichani hapo juu unaonyesha mfumo huo utakavyokuwa kwenye eneo la Manzese. Mamlaka inayohusika na usimamizi wa Ujenzi huo ya DARTS wamekua wakitoa maelezo kwa muda mrefu hassa kwenye maonyesho mbalimbali yanapofanuika lakini si aghalabu watu wote kuweza kufika.

Kwa mamtiki hiyo ningependa ndugu wasomaji muelewe yakuwa mfumo huo unaonekana pivhani ndiyo mfumo wenyewe utakavyokuwa, kwamaana kinachoonekana katikati ni kituo ambacho kisingi kitawahifadhi abiria wote wanaokwenda na kurudi mjini (Kariakoo, Posta na Fery) na mabasi yaendayo kasi yatasimama kulia na kushoto mwa kituo kutegemea na liendako.

Usafiri utakuwa ni bora zaidi kwasababu abiria watalipa nauli kabla ya kupanda basi, watapumzika kwenye kituo bila ya kuunguzwa na jua na barabara ya mabasi hayo yatakuwa yakipita yenyewe tu bila kuingiliana na magari mengine na kutoa fursa ya mwendo wa kasi.
Kuhusu magari mengine kama inavyoonekana pichani pembeni kabisa kutakuwa na barabara kwajili ya magari mengine ya kawaida huku kukiwa na sehemu maalum kwaajili ya kuvuka watembea kwa miguu”
****

Blog hii iliweza kutembelea maeneo tofauti ambako shughuli za ujenzi zinaendelea eneo la Ubungo hadi Magomeni chini ya wataalamu wa Kampuni ya STRABAG. Picha zifuatazo zinaonesha baadhi ya matukio ya kazi zinazoendelea..

DSCN4153DSCN4154DSCN4177DSCN4178DSCN4152DSCN4148

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

ray njau said...

Hakika penye nia pana njia.

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO