Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Wajasiriamali mikoa ya Kaskazini wapatiwa soko

TATIZO la kufikia vituo vya masoko na kuuza bidhaa kwa wajasiriamali wadogo na wakati, hasa wale wanaosindika vyakula, limepatiwa ufumbuzi kwa kuwawezesha kujua mahali lilipo soko husika kwa urahisi zaidi kwa gharama ya dola za Marekani 100 ambazo ni sawa na sh 158,000.

Kutatuliwa kwa kero hiyo kumebainishwa kuwa kutaleta ufanisi zaidi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati wanaosindika na kuuza vyakula nchini.

Hayo yalibainika wakati wa kuutambulisha mfumo wa taarifa za vituo vya masoko kwa wafanyabiashara wa Kanda ya Kaskazini mjini hapa jana na Meneja Biashara wa Mfuko wa kukuza ushindani kwa wajasiriamali wadogo na wakati (SCF) wa kanda hiyo, Michael Bulemo.

“Mfumo huu utamsaidia mjasiriamali kujua apeleke katika soko lipi bidhaa zake na kwa wakati gani. Lakini pia tunalenga kutoa elimu ya masoko ili kupunguza uingizaji wa bidhaa za usindikaji kutoka nje ya nchi,” alisema Bulemo.

Alisema mpaka sasa tayari SCF imefanikiwa kukusanya taarifa za kibiashara za vituo 14,904 ambavyo wajasiriamali hao wanaweza kufanya nao mazungumzo ya kibiashara kwa ajili ya kujua soko na hatimaye kuuza bidhaa husika.

“Mfumo huo utamuwezesha mjasiriamali kujua taarifa za mteja anayetaka kumuuzia bidhaa kwa kutumia mtandao ulioanzishwa kwa gharama ya dola za Marekani 100 ambazo ni sawa na sh 158, 000. Hii itampunguzia mjasiriamali gharama ya kufanya utafiti wa masoko,” alisema Bulemo.

Mwenyekiti wa kikundi cha ushirika wa Maziwa Wanawake cha wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro (Kalali), Nancy Manase, alisema kuwa kutambulishwa kwa mfumo huo kumefungua zaidi akili zao kibiashara

Source: Tanzania Daima

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO