Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Stashahada ya Uzamili ya Ujasiriamali yaanzishwa Arusha

Na Happy Lazaro, Arusha

CHUO cha Eastern and Southern African Management Instititute (ESAMI) kilichopo mjini hapa kimezindua kozi mpya ya Stashahada ya Uzamili ya Ujasiriamali ambayo itakuwa ikitolewa kwa kipindi cha miaka miwili.

Akizindua kozi hiyo chuoni hapo jana, Mkurugenzi Mkuu wa chuo hicho, Profesa Bonard Mwape alisema kuwa kozi hiyo ni ya tofauti sana tofauti na nyingine kwani inafanyika kimataifa zaidi na baada ya kuhitimu

wanafunzi wataweza kwenda kujiajiri wenyewe.

Alisema kuwa, wao kama chuo cha Esami wakishirikiana na Lund University walishirikiana kwa pamoja katika kuangalia uwezekano wa kuanzisha kozi hiyo ambapo wamekwishaanza na wanafunzi 25 tayari.

Alisema kuwa, kozi hiyo imekuwa ikifanyika kwa vitendo zaidi katika kuhakikisha kuwa wanawajengea uwezo wanafunzi hao kuweza kufanya biashara zao na kupata kipato ambacho kitaingizia taifa letu faida kubwa.

Aliongeza kuwa tatizo la Waafrika walio wengi wanapenda sana kuiga maswala ya nje ya nchi, wengi wao wakisubiri vitu mbalimbali vibuniwe nje ya nchi ndipo wanaenda kuvichukua na kuvileta huku hali ambayo aliipinga sana na kusema kuwa tunatakiwa sisi wenyewe tuwe wabunifu na kuwa na vitu vipya.

Profesa Mwape aliongeza kuwa, kupitia kozi hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuwa wabunifu zaidi na kuondokana na tabia ya kuiga vitu vinavyotengenezwa na wenzetu wa nje ya nchi badala yake ifike wakati sasa sisi ndio tuwe wabunifu na kuwa mfano wa kuigwa.

“Baada ya kozi  hii tunatarajia wajasirimali wetu watakuwa wabunifu wa kimataifa na hata kuwa mfano wa kuigwa na wenzetu wa nchi za nje, hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa wanajiunga na kozi hiyo kwani wakishatoka hapa wanajitegemea na sio kutafuta ajira tena,” alisema Profesa Mwape.

Kwa upande wake, Mkurugenzi katika Kituo cha Ujasirimali na Ubunifu ndani ya chuo cha ESAMI, Leon Malisa alisema kuwa, kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakitoa kozi ya utawala hivyo kwa sasa wameona ni vyema watoe ya ujasirimali ili kupunguza umaskini unaosababishwa na wanafunzi walio wengi kusubiri kuajiriwa pindi wanapohitimu masomo yao.

Alisema kuwa, wanafunzi walio wengi wakishahitimu masomo yao wamekuwa wakiishia kutokuwa na ajira kutokana na kushindwa kujiajiri, hivyo kupitia kozi hiyo wataweza kujiajiri wao wenyewe na hatimaye kupunguza umaskini.

Malisa alisema kuwa, baada ya mafunzo hayo wahitimu hawataondoka na vyeti tu, bali itawasaidia kuondoka na biashara za kimataifa ambazo zinawatoa kimaisha.

Alisema kuwa, darasa la kwanza walianza Jumatatu ya Mei 28 ambapo kwa darasa la pili wataanza rasmi Januari mwakani , ambapo wanafunzi wanaochukua kozi hiyo ni kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Zimbambwe na Malawi.

Aidha aliwataka wanafunzi mbalimbali kujitokeza kujiunga na mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwatoa kimaisha na kuweza kujiajiri, hali ambayo itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuongeza pato la Taifa.

Mwisho.

Chanzo: Mwananchi

June 06, 2012
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO