JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA
Tel: +255 22 21122065/7
Fax No. +255 22 2112538
Email: tanzparl@parliament.go.tz
Ofisi ya Bunge
S.L.P. 941
DODOMA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
06.06.2012
YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013
Ndg. Waandishi wa Habari
Mwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake katika Bajeti Mbadala
ambavyo vilikuwa:
1. Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%
2. Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili kupunguza mfumuko wa bei
3. Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).
4. Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye bodi ya mikopo
ya elimu ya juu.
Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti kivuli iliyowasilishwa Bungeni na
Kambi ya Upinzani.
Mapendekezo mawili,
(1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na
(2) Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa lakini
Serikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo la kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.
Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali imeshindwa kutekeleza ahadi
yake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya kodi itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa.
Halikadhalika Kambi ya Upinzani inarejea wito wake wa kufutwa kwa Mfumo wa posho za vikao
(sitting allowances).
Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs. 15trillioni kutoka Tshs. 13 trillion. Hata hivyo ni dhahiri
kwamba Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezaje
kutekeleza Bajeti ya 15trillioni?
Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika maeneo yafuatayo na
kuishinikiza Serikali kuyatekeleza.
1. Kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya Pato la Taifa. Hivi sasa
misamaha ya kodi ni sawa na misaada yote kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni sawa na 3% ya
Pato la Taifa.
2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga miundombinu kama barabara za
vijijini na umeme vijijini.
3. Kuelekeza fedha za kutosha kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia za Reli za Tanga, Moshi na
Arusha.
4. Kuongeza wigo wa kutoza tozo la ujuzi (Skills Development Levy) ambapo sasa waajiri wote
walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma. Pia kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3
itaenda VETA na vyuo vya Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto ya
mikopo kwa wanafunzi.
5. Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9% ili kuwezesha wananchi wa hali
ya chini kubaki na fedha za kutumia na kukuza uchumi.
6. Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa kuhakikisha mapato ya ndani
yanafikia 20% ya pato la taifa, kuongeza nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidi
kwenye kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mafuta na gesi.
7. Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.
8. Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili kushusha mfumuko wa
bei.
9. Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa elimu kwa ubora zaidi,
ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa Elimu(Regulatory authority)
10. Kutoa vipaumbele na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi za nchni
hasa za kilimo na zenye kuongeza ajira kama Korosho,Pamba na Mkonge.
Kambi ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua kwa deni la Taifa amabalo
limefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi maalum kuhusu akaunti ya Deni la Taifa.
Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi yasiyo na tija ya Serikali hasa
kwenye magari na posho mbalimbali na Kwamba fedha nyingi zitumike kwa miradi mikubwa ya
maendeleo ili kukuza ajira. Halikadhalika namna ya kupta fedha za kutekeleza mpango wa
Maendeleo wa Miaka mitano
Asanteni sana!
…………………………….
Zuberi Kabwe Zitto(Mb)
Waziri Kivulu-Fedha na Uchumi.
0 maoni:
Post a Comment