Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Taswira za mkutano wa CHADEMA eneo la Kia, Kilimanjaro Juni 10, 2012

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeendelea na mikutano yake ya hadhara katika Wilaya ya Hai kwa kufanya mkutano mwingine eneo jirani na uwanja wa Kimataifa wa ndege KIA juzi.

Mkutano huo ulioratibiwa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Wilaya ulihudhuriwa na baadhi ya ‘makamanda’ wa chama hicho tokea mkoani Arusha baadhi wakiwa wasemaji waalikwa.

Pamoja na mambo mengine, tatizo la ajira kwa wenyeji wa eno la uwanja na mishahara hewa liliibuliwa katika mkutano huo.

Mjumbe wa Kamati tendaji Wilaya wa chama hicho, Ndg Joseph Shao maarufu kama Kimeta wa Mererani aliibua tuhuma hizo na kulalamika kuwa wageni ndio wamekuwa wakipata ajira katika uwanja huo wa na kwamba wenyeji wangepaswa kupewa kipaumbele.

Bw Shao aligusia pia uwepo wa watumishi ambao hawapo kazini kwa zaidi ya miaka 10 lakini bado mishahara yao inatoka nakuliwa na wajanja wachache bila kuwafikia wahusika.

DSCN3770 Joseph Shao, mjumbe wa Kamati tendaji CHADEMA Wilaya ya Hai akihutubia

DSCN3808

DSCN3800Kamanda wa CHADEMA toka Arusha, Magoma Jr Magoma alifafanua mapungufu yaliyopo katika utekelezaji wa ilani ya CCM

DSCN3758 Benchi la viongozi na wananchama waalikwa mkutanoni hapo

DSCN3730 Hapa ni kabla safari ya kwenda Kia tokea Arusha haijaanza…

DSCN3762 Anaitwa Doris Cornely. Mwanadada huyu aliwahimiza wananchi hao wa Kia kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na pia kushiriki katika mchakato wa kuandika Katiba mpya ya nchi pindi muda ukifika.

DSCN3833   Mwananchi huyu aringishia kadi yake mara baada ya kuilipia na kukabidhiwa

DSCN3844Vijana wa BAVICHA toka Arusha ambao waliamua kufanya safari kuungana na wenzao wa Hai katika mkutano huo. Kutoka kushoto, Hassan Noor, Moses Joseph, Doris Cornely, Zion William, Emmanuel Saro na mkulu wa blog hii akiwachombeza mawili matatu.

DSCN3837Mwenyekiti wa Baraza la Wananwake CHADEMA Wilaya ya Hai, Bi Mamuu Daud Lole akilalamikia makosa yaliyofanywa na NECTA katika utoaji matokeo ya Somo la Kiislamu na kuwafelisha wanafunzi ambavyo haikustahili. Anaezungumza nae ni Ndg Calist Bush, aliekuwa Mwenyekiti wa TLp Wilaya ya Arusha kabla ya kujiunga na CHADEMA mapema mwaka huu.

DSCN3930Kamanda wa Vijana CHADEMA Arusha, ambae pia ni mwanasheria, James Lyatuu akimuelekeza namna ya kufanya ishara ya “v” mwananchama huyu mpya Christina Mtuha aliekuwa miongoni mwa watu kumi walionunua kadi za uanachama pale Big L Pub wakati makamanda hao wakiwa wamefika hapo kujipongeza

Picha zote na maelezo: Tumainiel Seria

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

shagihilu said...

Safi sana hakuna kulala mpaka kieleweke

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO