Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

‘Kondakta mzungu’

DSCN3399

Kamera ya Blog hii ilibahatika kunasa tukio hili juzi asubuhi maeneo ya Kijenge Mwanama ambapo raia hawa wa kigeni walilazimika kuning’inia mlangoni mwa daladala hili kama inavyoonekana, jambo ambalo ni kinyume na sheria za usalama barabarani na ni hatari pia kwa maisha yao. Daladala hili lilikuwa likitokea Moshono kwenda Mjini Arusha. Kwa miezi ya karibuni kumekuwa na tatizo la usafiri hususani majira ya asubuhi na jioni hatua inayolazimu abiria wenye haraka kujibana kwa nafasi ndogo inayopatikana na wengine kuamua kubaki nje kama hawa.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO