Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Madaktari waunda jopo kumuokoa Dr Ulimboka

419324907 Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, akiwa kwenye Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI). (Picha na Deus Mhagale)

MADAKTARI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wameunda jopo maalumu la madaktari kwa ajili ya kumtibu Mwenyekiti wa Jumuiya wa Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, aliyejeruhiwa juzi usiku, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana.

Jopo hilo, liliundwa jana na timu ya madaktari hao, ambao kwa kauli moja walimchagua Profesa Joseph Kihamba kuwa kiongozi wao hadi Dk. Ulimboka atakapopona.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, kuhusu hali ya Dk. Ulimboka, Profesa Kihamba alisema hivi sasa anaendelea vizuri na ameanza kuzungumza.

Alisema licha ya Dk. Ulimboka kuendelea vizuri, bado yupo Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) na madaktari wanahaha namna ya kuokoa maisha yake.

“Mie sio mzungumzaji, lakini kwa ufupi napenda kuwaeleza Watanzania, madaktari na jamii yote kwamba afya ya Dk. Ulimboka, imeanza kuimarika … madaktari tupo bega kwa bega kuhakikisha anapona haraka na hivi sasa ameanza kuongea.

“Jopo hili, lililoundwa limeaminiwa na madaktari wengine…sisi tutafanya kazi kadri ya uwezo wetu, ili kuhakikisha mwenzetu anapona haraka, tutakuwa naye muda wote,” alisema.

Naye Msemaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Jumaa Almasi pamoja na kuelezea hali ya Dk. Ulimboka, alisema huduma zimezidi kudorora katika vitengo mbalimbali ndani ya hospitali hiyo.

Alisema huduma zimesitishwa katika vitengo mbalimbali, isipokuwa dharura, huku wagonjwa wakizidi kuchukuliwa na ndugu zao na kuwapeleka katika hospitali nyingine, hususan za binafsi.

“Dk. Ulimboka anaendelea vizuri na huduma anapata kama inavyopaswa, lakini ninachoweza kuwaeleza ni kwamba tangu mgomo utangazwe huduma hapa zimekuwa za kusuasua na baadhi ya vitengo vimesitisha kabisa, isipokuwa dharura.

“Baadhi ya wagonjwa wengine bado wapo hapa hospitalini na wanaendelea kupata tiba, ingawa ni ya kusuasua kutokana na hali hii, na kibaya zaidi hivi sasa madaktari hawaonekani kabisa hapa, sasa inakuwa kazi ngumu,” alisema.

Source: Gazeti Mtanzania, 29 Juni, 2012

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO