Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Breaking News: Vijana wa kitanzania wafariki ajalini Kenya, yumo mtoto wa Mchungaji wa EAGT Arusha

Blog hii imepokea taarifa ya kusikitisha usiku huu kutoka vyanzo vyake vya kuaminika ikieleza kuwa kuna ajali mbaya ya barabarani imetokea jioni ya leo na kupelekea vijana watatu wa kitanzania, wakazi wa Arusha kupoteza maisha na wengine ambao idadi yao haijajulikana kujeruhiwa vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, ambazo bado hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi, vijana hao wamepata ajali nchini Kenya wakiwa njiani kurejea Arusha kutokea Jijini Nairobi wakitumia gari binafsi.

Vijana waliotajwa kufariki katika ajali hiyo mbaya ni Faraj Haule ambae ni mtoto wa Mchungaji Marko Haule, wa Kanisa la EAGT Elerai, Arusha na Denis Ngalesoni ambae ni mtoto wa mmiliki wa shule ya Green Acres ya Jijini Arusha.

Mwingine majeruhi ambae jina lake halijaweza kutambulika mapema, anaelezwa kuwa ni mtoto wa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, maarufu kwa jina la Sunda.

Blog hii inatoa salamu za pole kwa wafiwa, na kumuomba Mungu aziweke roho za marehemu hao mahali pema peponi, na kuwapatia nafuu ya kupona majeruhi wote!

Tunaendelea kufuatilia zaidi..

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

4 maoni:

Lucci said...

Jamani numehuzunika sana , Dennis alikua school mate wangu, very young, may their souls rest in peace

Anonymous said...

Sio mtoto wa Sunda ni mtoto wa jungle master anaitwa victor pia mtoto wa makoye anaitwa simon

Unknown said...

Nashukuru kwa ufafanuzi. Karibu

Anonymous said...

Jamani hyo sio mpaka umwambie mtu afunge news zina kuja in many ways hata mi at first niliambiwa kafa na watu wakawa wame post picha za 3 people.Nice blog thanks 4 da news ila walio kufa ni wawili da two wako okay simon na victor

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO