Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Waapishwa!

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo wameapishwa rasmi kushika madaraka hayo huku Tanzania ikiwa na Wawakilishi tisa katika Bunge hulo.

Wabunge hao waliapa baada ya kupatikana Spika wa mpya wa Bunge hilo ambapo safari hii ikiwa ni Uganda kushika Uongozi huo wa Juu wa Bunge na Mwana Uchumi, Margareth Zziwa kuchukua nafasi hiyo.

Wabunge wote wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki waliokula kiapo hii leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania kwenye Bunge EALA, Alhaj Adam Omar Kimbisa na Katibu wake, Mh Shy-Rose SaddrudinBhanji.

Wengine ni Mhe. Anjela Charless Kizigha, Mh. Maryam Ussi Yahya,Mh.Nderkindo Perpetua Kessy, Dkt Twaha Issa Taslima, Mhe. Abdullah Ali Hassan Mwinyi, Mhe Bernard Musomi Murunyana Mhe. Charles Makongoro Nyerere na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta anaeingia kwa wadhifa wake wa Uwaziri.

Wabunge hao wameapisha pamoja na wabunge wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda.

EALAShy- Rose Banji akila kiapo

EALA1 Mhe. Samuel Sitta ni mwakilishi wa Tanzania, Wizara ya Afrika Mashariki.

EALA2 Mhe.Abdullah Alli Hassan Mwinyi.

EALA3Mhe. Charles Makongoro Nyerere.

EALA5Dkt. Twaha Issa Taslima.

EALA4Mhe. Alhaji. Adam Kimbisa.

EALA6 Mhe.Nderkindo Perpetua Kessy.

EALA7 Mhe. Bernard Musomi Murunyana.

EALA8Mhe. Anjela Charless Kizigha, akila kiapo.

Picha na maelezo: FATHER KIDEVU

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO