Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Barua inayodaiwa kunandikwa na Watanzania wafungwa wa dawa za kulevya Hong Kong ikiwataja vibosile wa biashara hiyo nchini hii hapa!!

Ijapokuwa hizi ni tuhuma tu, lakini kusikia majina yaliyotajwa katika “barua kutoka Hong Kong” kwa miongoni mwa watanzania wanaosemekana kufikia hata 200 wanaosota katika jela za nchini humo  kusikia majina ya watu waliotajwa katika waraka huo ambao bila shaka utapamba vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wiki kadhaa zijazo ni jambo zito kidogo.

Barua hiyo (ambayo utaisoma hapa chini) inahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina. Lakini kutokana na ukweli kwamba imeainisha watu wanaosadikiwa kuhusika, bila shaka imelipa jeshi la Polisi mahali pazuri pa kuanzia. Je,wanaotajwa kipato chao kinatokana na biashara gani zilizo halali? Ukaguzi wa vitabu vyao vya fedha unasemaje?

Miongoni mwa majina hayo, limo jina la Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh Iddi Azan.

Jambo moja ambalo linasikitisha sana (endapo tuhuma hizi zitathibitishwa hususani kumhusu Iddi Azan) ni kwamba Jimbo au Wilaya ya Kinondoni ni miongoni mwa maeneo ambayo yanaongoza kwa vijana kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.Je,ina maana Mbunge wake anahusika katika kuangamiza vijana au wapiga kura wa jimbo lake mwenyewe?

 

SOMA BARUA YENYEWE HAPA CHINI…
baruamadawa(01)
baruamadawa(02)
baruamadawa(03)
baruamadawa(04)
baruamadawa(05)
  Chanzo - Bongo celebrity

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO