Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

CHADEMA YAITESA CCM UCHAGUZI UDIWANI ARUSHA, YAKOMBA KATA ZOTE NNE KWA KISHINDO

Polisi wakimsihi Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari aondoke nje ya kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya kata ya Kimandolu,pamoja na makada wa CCM hawako pichani ambapo walitakiwa kukaa mita 200 badala ya mita 100. (Picha zote na Ferdinand Shayo)

Polisi wakimsihi Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari aondoke nje ya kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya kata ya Kimandolu,pamoja na makada wa CCM hawako pichani ambapo walitakiwa kukaa mita 200 badala ya mita 100.

Makarani wa uchaguzi wakiingiza masanduku ya kura katika ofisi ya kata ya Kimandolu kutoka kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi kimandolu.

Makarani wa uchaguzi wakiingiza masanduku ya kura katika ofisi ya kata ya Kimandolu kutoka kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi kimandolu.

Polisi wakiimarisha ulinzi katika lango kuu la kuingilia kituo cha kupigia kura cha Ofisi ya kata ya Kimandolu katika uchaguzi ulifanyika leo mjini Arusha.

 

Zoezi la kupiga kura likiwa limekamilika majira ya saa kumi jioni na kiukweli inasikitisha kuona ni idadi ndogo ya wananchi wapiga kura wamejitokeza kupiga kura.



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), `kimefunika' katika uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika kwenye kata nne za Jimbo la Arusha Mjini uliofanyika jana.

Matokeo katika vituo mbalimbali vya kata hizo nne ambayo kwa mujibu wa   Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), yalionyesha Chadema ikiongoza kwa idadi kubwa ya kura zilizopigwa kwenye vituo 136 vya kupigia kura huku kikifuatiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Matokeo kamili katika vituo hivyo yalikuwa kama ifuatavyo:-

KATA YA KALOLENI:
Matokeo ya jumla Chadema 1,470, CCM 530, CUF 275 na Demokrasia Makini 2,  Kwa matokeo hayo Emmanuel Kessy wa Chadema alitangazwa mshindi.
Kituo kidogo A, Chadema kilikuwa kimenyakua kura 51, CCM 25 na CUF 11.
Kituo B1, Chadema 68, CCM 19 na CUF 17 huku katika kituo A4, Chadema kilipata kura 67, CCM 20 na CUF 9, Kituo A3 Chadema kura 57, CCM 25 na CUF 7.
Katika kituo cha B4, Chadema kura 54, CCM 30 na CUF 9, B3 Chadema 54, CCM 15 na CUF 9, wakati B2 Chadema kilipata kura 73, CCM 9 na CUF 4 na kituo A2, Chadema 69, CCM 21 na CUF 8.
Kituo cha A1, Chadema kura 60, CCM 15 na CUF 11 na B6 Chadema kura 41, CCM 21 na CUF kura 9.
Katika kituo cha B5, Chadema kilipata kura 50, CCM 22 na CUF 10.
Katika kituo cha AICC Nursery School, kituo kidogo cha A2 Chadema kura 58, CCM 18 na CUF 17, A4 Chadema kura 62, CCM 22 na CUF 6, A3 Chadema 44, CCM 22 na CUF 5, E2 Chadema 58, CCM 22 na CUF 4, E3 Chadema 53, CCM 20 na CUF 5.
Aidha, katika kituo cha E4 Chadema 40, CCM 20 na CUF 5, B1 Chadema 57, CCM 18 na CUF 9, A1 Chadema 60, CCM 24 na CUF 5.
Kituo cha Shule ya Sekondari Kaloleli, A1,Chadema 52, CCM 17, CUF 15 huku katika kituo cha A2, Chadema kura 97, CCM  23,  CUF 19 na kituo A3, Chadema 46, CCM 20 na CUF 20.
Kituo cha A4 Chadema 46, CCM, 16, CUF 16, kituo B1 Chadema 56, CCM 10, CUF 16 na kituo B2 Chadema 42, CCM 23 na CUF 15.
Kituo B3, Chadema 53, CCM 17  na CUF 11, kituo B4 Chadema 38 CCM 16 na CUF 13
KATA YA ELERAI
Katika Kituo cha Shule ya  Sekondari Kata ya Elerai, Ofisi ya Katibu Tarafa, pia Chadema kimeendelea kuongoza katika matokeo ya awali.
Matokeo ya jumla Chadema kura 2,047, CCM 1,471, CUF 302, CCK 3, na TLP 1. Mshindi ni Mhandisi Jeremiah Mpinga wa Chadema.
Kituo A1, Chadema kura 37, CCM 17, CUF 3, TLP na CCK 0. Kituo A2, Chadema kilipata kura 28, CCM 13, CUF 2, CCK na TLP 0.
Kituo A3, Chadema kura 31, CCM 19, CUF 2, CCK na TLP 0 huku katika kituo A4 , Chadema 21, CCM 12, CUF 6 , TLP na CCK 0.
Vituo vingine katika kata hiyo ni pamoja na B1 ambacho Chadema waliongoza kwa kura 42, CCM 15, CCK na TLP 0 huku katika kituo C1, Chadema 42, CCM 15, CCK na TLP 0.
Kwa upande wa kituo cha C2, CCK 0, CCM 12, Chadema 35, CUF 3 na TLP 0, Kituo kingine cha Katibu Tarafa Ofisi, CCM kilipata kura 26, Chadema 25 na CUF huku cha B1 Chadema wakijipatia kura 43, CCM 23, CUF 5.
Kituo B2, Chadema 34, CCM 24, CUF na TLP 0, kituo B3  CCM kura 26, Chadema 32, CUF 3, kituo cha Shule ya Msingi Burka B2, CCM ilinyakua kura 31, Chadema 30, CUF 2 na kituo B3, CCM ikipata kura 41, Chadema 43, CUF 5 wakati CCK na TLP wakiambulia patupu.
Aidha katika kituo hicho cha Shule ya Msingi Burka,B4 CCM ilipata 32, Chadema 28, CUF 3, TLP na CCK 0, vituo vya C1, CCM kura 26, Chadema 43, CUF 5 na kile cha C2, CCK 0, CCM 31, Chadema 43, CUF 7 na TLP 0.
KATA YA KIMANDOLU
Katika Kata ya Kimandolu kwenye kituo Shule ya Msingi Suye, CCM na Chadema ndivyo pekee vilisimamisha wagombea.
Katika kituo cha A1, CCM ilipata kura 15, Chadema 47, A2  CCM 24, Chadema 39, kituo A3 CCM 14, Chadema 35,  kituo B1 CCM 25, Chadema 56,  kituo B2 CCM 25, Chadema 48, kituo C2 CCM 30, Chadema 39 na kituo C1 CCM 11, Chadema 48.
Kituo cha ofisi ya Kata ya  Kimandolu, kituo A1 Chadema ilipata kura 97, CCM 22,  kituo A2  Chadema 88, CCM 29, kituo A3 Chadema 81, CCM 31, kituo A5 Chadema 90, CCM 41, kituo A6 Chadema 87, CCM 28, kituo A7 Chadema 70, CCM 35,  kituo B1 Chadema 84, CCM 27 na kituo B2 Chadema 82, CCM 27.
Kituo B3 Chadema 78, CCM 37, kituo B4 Chadema 87, CCM 36, kituo cha B5 Chadema 69, CCM 23, kituo C1 Chadema 97, CCM 28, kituo C2 Chadema 103,CCM 21, kituo C3 Chadema 79, CCM 32, kituo C4 Chadema 84 CCM 42 na kituo C5 Chadema 87 CCM 41.
Kituo cha Shule ya Msingi Kimandolu kwenye kituo A1 CCM ilipata kura 34, Chadema 64, kituo B2 CCM 26, Chadema 66, kituo B4 CCM 37, Chadema 74, kituo A5 CCM 48, Chadema 58, kituo A3 CCM 48, Chadema 53, kituo B5 CCM 24, Chadema 65, kituo C1 CCM 27, Chadema 74, kituo C3 CCM 36, Chadema 64, kituo C5 CCM 31, Chadema 78, kituo A2 CCM 27, Chadema 87, kituo A4 CCM 33, Chadema 57, kituo B2 CCM 30, Chadema 77 na kituo C2 CCM 30,Chadema 65.
KATA YA THEMI
Katika kata hiyo iliyokuwa na vituo 12, Chadema ilinyakua jumla ya kura 674, CCM 326 na CUF 307. Waliojiandikisha walikuwa 6,387, waliopiga kura 1,319, kura halali 1,307 ambapo zilizoharibika 12, kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi wa kata hiyo, Eveka Mboya ambaye pia alimtangaza mshindi kuwa ni Kinabo Edmund wa Chadema.
Matokeo kwa baadhi ya vituo yalionyesha kuwa katika Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa  Kata ya Themi, CCM  9, Chadema 36, CUF 0, kituo A2 CCM kura 13, CUF 3 na Chadema 23, kituo cha A3 , Chadema 33, CCM 16, CUF 2 na katika kituo A1, CCM ikijipatia kura  44, CUF 1, Chadema 53.
Katika kituo A2, CCM 29, Chadema 57 na CUF 4 huku kile cha A3 CCM ikijipatia kura 23, Chadema 44 na CUF kikiambulia 0.
Kata ya Themi ilikuwa na vituo 12 ambapo hadi tunakwenda mitamboni matokeo ya vituo sita yalikuwa yamepatikana huku matokeo ya vituo vingine yakiendelea kuhesabiwa.

 
HALI ILIVYOKUWA KABLA
ULINZI
Awali, ulinzi mkali wa polisi waliokuwa wamevalia sare na kiraia, ulikuwa umeimarishwa maeneo ya vituo vya kupigia kura vya kata za Themi, Kimandolu, Kaloleni na Elerai, ambako kulifanyika uchaguzi huo.
UTATA WA VITAMBULISHO
Katika Kata ya Kimandolu, watu wawili walikutwa na  kadi za kupigia kura zisizo za kwao, mojawapo ikiwa na taarifa zisizo za mhusika huku picha ya kitambulisho ikionyesha yake.
Aidha, kati ya wapiga kura hao, mmoja alijulikana kwa jina la Mariamu, ambaye alikamatwa kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Kimandolu, saa 3.10 asubuhi, ambapo huyo alikutwa na kitambulisho chenye rangi, badala ya cheusi na rangi nyeupe na kutiwa mbaroni.
Mpiga kura mwingine ambaye jina lake kupatikana, alibambwa na kitambulisho feki kituo cha Ofisi ya Mtendaji, kituo kidogo C5, ambapo alikuwa kijana aliyetoa kitambulisho chenye taarifa zisizo zake, huku picha ikiwa ya mpiga kura.
Hata hivyo, kijana huyo hakukamatwa baada ya kukimbia.
Akizungumzia hali hiyo ya kukutwa na vitambulisho feki, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba na Mkuu wa Jopo la waangalizi wa uchaguzi, Deus Kibamba, alisema suala la watu kukutwa na vitambulisho feki linapaswa kuchunguzwa kwa undani na siyo la kulipuuza.
“Hili suala zito na linahitaji kufuatiliwa, badala ya kupuuza kufahamu chanzo cha vitambulisho hivyo ili demokrasia iwe huru,” alisema.
Kuhusu suala la wapiga kura kutojitokeza kwa sababu za ulinzi wa Polisi kuimarishwa, Kibamba alisema hilo kwake haliwezi kuwa sababu, isipokuwa kitu kikubwa wanachoona uwapo wa askari umesaidia kuimarisha amani.
“Lakini kikubwa wenzetu tumewaomba wa usalama na Polisi, wakae pembeni bila kusumbua watu kwa kuwatisha ili wapiga kura wasiogope kupiga kura,” alisema.
Alisema kuwa katika uchaguzi huo, kikubwa kimejitokeza suala  la wapiga kura kukaa umbali wa mita 100.
“Mimi nasema hili la mita 100 sheria ipo wazi inasema watu wakipiga kura wakae mita 100 ili waone kinachoendelea na kusherehekea mshindi atakayepatikana, lakini kushauri watu wasikae kwa sababu ya huruma ya kuungua jua, hilo ni suala lingine,” alisema Kibamba.
Msimamizi wa uchaguzi wa Chadema,  Alphonce Mawazo, alisema amesikitishwa kuona askari wamemwagwa wengi, huku kukiwa hakuna sababu za msingi za kufanya hivyo zaidi ya kuwatisha wapiga kura.
“Kawaida askari wanatakiwa waje hapa vituoni muda wa kuhesabu kura na siyo asubuhi, hii imechangia kutisha watu kwa kuwalazimisha kukaa mita 200, kitu ambacho kinyume cha sheria,” alisema.
Mawazo alisema kuwa wasiwasi wanaopata ni kuwapo kwa timu ya watu mbalimbali wasioruhusiwa na Tume kuingia eneo la kuhesabia kura, ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Kimandolu bila sababu za msingi.
Lakini alisema idadi ya watu wachache imejitokeza.
Msimamizi wa Uchaguzi wa ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Kimandolu wa CCM, Abraham  Joseph,  alisema idadi ya wapiga kura siyo wengi na waliojitokeza ni vijana lakini kwa wazee na wa akina mama walikuwa wachache kutokana na hofu waliyonayo ya vurugu zilizotokea siku za nyuma.
Kuhusu uwapo wa polisi wengi vituoni, alipongeza kuwa unadumisha  amani lakini alilalamikia suala la baadhi ya wapiga kura kukutwa na vitambulisho feki.


Alisema kuwa Kata ya Kimandolu ina wapigakura zaidi ya 12,000, lakini kwa idadi ya wapiga kura inavyojitokeza chache ana shaka kama itafikia hata watu 4,000 watakaopiga kura.
Kwenye kata ya Elerai, mtu mmoja, Zainabu Maulid, alikamatwa na polisi katika kituo cha kupigia kura cha Sekondari ya Elerai, akiwa na kadi ya mpiga kura iliyokuwa imebandikwa kienyeji.
Kadi hiyo ilizua utata kwa mawakala na makarani na polisi walilazimika kumchukua hadi kituoni bila kupiga kura.
­­­Mapema, saa 12:00 asubuhi, Hassan Noor, aliyedai kuwa ni wakala msaidizi wa Chadema pamoja na mwenzake aliyemtaja kwa jina la Bonny, walishambuliwa na kundi la watu waliokuwa kwenye gari aina ya Land Cruizer iliyokuwa na rangi ya maziwa.
Alisema tukio hilo lilitokea jirani na kituo cha kupigia kura cha Nursery kilichopo eneo la Soweto Kata ya Kaloleni ambapo alichaniwa barua yake ya utambulisho wa kuwa wakala.
Alisema alitoa taarifa kuhusu tukio hilo kwa polisi waliokuwapo eneo la kituo hicho na kwa msimamizi msaidizi. Alidai kuwa watu hao walimpiga kwa kitu kizito mwenzake.
Lakini uchunguzi uliofanywa na NIPASHE uligundua kuwapo kwa kasoro kadhaa katika vituo hivyo zilizosababisha mamia ya waliokuwa wakitaka kupiga kura kushindwa kufanya hivyo.
Wengi walishindwa kupiga kura kutokana na majina yao kutokuwapo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura licha ya majina hayo kuwapo kwenye orodha ya majina yaliyobandikwa kwenye mbao za matangazo katika kila ofisi ya Mtendaji wa Kata.
Wengine walishindwa kupiga kura kutokana na namba za kadi za kupigia kura katika kadi za vitambulisho vya kura kutofautiana na zile zilizopo kwenye daftari hilo.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kaloleni, Anna Lebisa, ambaye ndiye alikuwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi katika kata hiyo, alikiri kuwapo kwa baadhi ya wapiga kura  walioshindwa kupiga kura kutokana na majina yao kutokuwapo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura licha ya majina yao kuwapo kwenye orodha iliyobandikwa kwenye mbao za matangazo ofisini hapo.
Akizungumzia tatizo hilo, alisema ilikuwa ngumu kuwasaidia watu ambao majina yao hayakuwapo kwenye daftari hilo kwa sababu ya sheria hairuhusu kufanya hivyo.
“Ni vigumu kuthibitisha kama kadi ya mpiga kura anayokuonyesha ni halisi au feki…tunachoangalia zaidi ni majina na picha vilivyomo kwenye daftari ambalo ndilo la uhakika zaidi.
“Kama kuna mtu ambaye jina lake halimo kwenye orodha ya majina iliyobandikwa lakini ana kadi yenye picha na jina lake lipo kwenye daftari la kudumu, huyo anaruhusiwa kupiga kura kisheria.
“Lakini kwa mtu ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya majina yaliyobandikwa hapa ofisini na lipo pia kwenye daftari la kudumu isipokuwa namba zinatofautiana, hapo busara inatakiwa itumike,” alisema.
Msimamizi huyo alikuwa akitoa ufafanuzi kwa NIPASHE kuhusu kasoro zilizojitokeza katika kata yake zilizotolewa na wapigakura kadhaa.
Mpiga kura, Omar Othman Jamaa, alisema licha ya kuwa na kadi ya mpiga kura na jina lake kuwapo kwenye orodha ya ubaoni, lakini halipo katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Alisema kadi hiyo ni mpya ya mwaka 2010.
Hata hivyo, Omar alisema suala hilo amelifikisha kwa msimamizi msaidizi wa uchauguzi lakini alikiri kwamba hana maamuzi yoyote.
“Mtendaji hana maamuzi yoyote, kaniambia tu nizunguke kwenye vituo vyote kuangalia huenda jina langu litakuwapo kwenye moja ya kituo…nimefanya hivyo tangu asubuhi hadi sasa majira ya saa sita hivi bado sijafanikiwa,” alisema.
Mpiga kura mwingine, Richard Method Minja, alilaamikia tatizo katika kadi yake yenye namba 32479311 ambayo ni tofauti na ile iliyomo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ambako imeandikwa namba 23291201.
Alisema kadi yake ina picha yake halisi, kadhalika katika daftari hilo lakini hakuruhusiwa na makarani pamoja na mawakala kupiga kura.
Mgombea udiwani wa kata hiyo, Darwesh Ramadhan (CUF), alilalamikia mtoto wake kushindwa kupiga kura kutokana na jina lake kutokuwapo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.
Akizungumzia hali hiyo, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Julius Mallaba, ambaye yupo mjini hapa, alikubaliana na majibu yaliyotolewa na msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa Kata ya Kaloleni.


Kuhusu hali ya upigaji kura kwa ujumla, Mallaba alisema ilikuwa inaendelea vizuri.


Kulikuwa na pilikapilika nyingi za wapiga kura kutafuta majina yao kwenye orodha iliyokuwa imebandikwa kwenye mbao za matangazo katika ofisi za kata na baada ya kuyaona walikuwa na kazi ya kutafuta kituo cha kupigia kura ambako kulikuwa na mawakala na makarani na daftari la kudumu la wapiga kura.


Hata hivyo, idadi kubwa ya wapiga kura ilikuwa zaidi majira ya asubuhi na iliendelea kupungua kadiri muda ulivyokuwa ukisogea mbele.
Watu wenye ulemavu wa macho walionekana wakisindikizwa na ndugu zao ambao walikuwa wakiwasaidia kupiga kura.


KATA YA THEMI
Uchunguzi uliofanywa katika Kata ya Themi, ulionyesha kuwapo kwa hali ya amani wakati wa zoezi la upigaji kura.
Hata hivyo, kulikuwa na matukio ya kuwapo kwa kasoro kadhaa kwa baadhi ya wapigakura kutoyaona majina yao kwenye orodha ya majina iliyokuwa imebandikwa kwenye mbao za ofisi za kata na wengine majina yao hayakuwapo kwenye daftari la kudumu la wapigakura.
Akilalamikia suala la utata wa kutokuwapo kwa majina ya wapigakura akiwamo mgombea wa CUF wa kata hiyo, Lobora Ndarpoi,  alisema kuwa alikwenda sehemu alikokuwa amejiandikisha lakini hakukuta jina lake.


Hata hivyok, alisema baada ya maelekezo aliliona jina lake na baadaye kupiga kura.
“Usumbufu wa aina hii unaweza kuwafanya wapiga kura wengi kukata tamaa na hivyo kupoteza haki yao ya Kikatiba,” alisema.
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata hiyo ya Themi, Eveta Mboya, alisema majina ya wapigakura yalibandikwa takribani siku 30 na kuwa wananchi walishindwa kwenda kuhakiki.
Alisema usumbufu kama huo ni wa kujitakia kwani kama
wapigakura wangekwenda mapema kuangalia majina yao wangejua kituo gani wanatakiwa kupiga kura na wangepiga kura zao bila usumbufu wowote.


“Uhakiki ni jambo la muhimu ili kukwepa usumbufu wa kutoona jina siku ya kupiga kura," alisema.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini,  Amani Golugwa, alisema idadi ya wapigakura iliyojitokeza ilikuwa ni ndogo, na kuwasihi watu kuacha woga na kwenda kupiga kura.
Hata hivyo, Golugwa alipongeza Jeshi la Polisi kutoa ushirikiano mzuri kwenye vituo pale wanapohitajika kufanya hivyo na kuwaomba waendelee hivyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya uchaguzi iliyotolewa na Halmashauri ya Jiji la Arusha, kuna wapiga kura 60,123 waliojiandikisha ambapo Kata ya Kaloleni ina wapigakura 12,636, Elerai wapigakura 23,791, Kimandolu 17,294 na Themi 6,396.

HOFU YAKIMBIZA WAPIGA KURA

LICHA ya hujuma ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ufanisi mdogo wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka na ushindi mnono katika uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata nne za jijini Arusha.

Katika Kata ya Elerai, mgombea wa CHADEMA Injinia Jeremia Mpinga alimbwaga Emanueli Laizer wa CCM kwa kura 1,715, dhidi ya 1,239.

Kata hiyo ilikuwa na wapiga kura 23,797 waliojiandikisha na vituo 55 vya kupigia kura, lakini idadi kubwa ya wananchi hawakujitokeza.

Matokeo ya kura yalitangazwa chini ya ulinzi mkali wa askari polisi zaidi ya 40 wenye silaha, na kupokelewa kwa shangwe kubwa na wafuasi na mashabiki wa CHADEMA.

Katika Kata ya Kaloleni, mgombea wa CHADEMA, Kessy Emmanuel Miliare alimshinda kwa mbali mgombea wa CCM kwa kura 1,470 dhidi ya 530, wakati mgombea wa CUF ameambulia kura 275. waliojiandikisha 12,674 waliopiga kura 2,292. Kura halali ni 2,277 na zilizoharibika 15.

Akitangaza matokeo katika Kata ya Themi, Msimamizi wa Uchaguzi, Editha Mboye alimtangaza mgombea udiwani wa CHADEMA, Mallance Kinabo kuwa mshindi kwa kupata kura 678, akimwacha mbali mgombea wa CCM Victor Mkolwe aliyepata kura 326, huku yule wa CUF, Lebora Ndervai akipata kura 313.

Kata ya Kimandolu, CHADEMA pia wameibuka na ushindi mkubwa na kuiacha vibaya CCM.

Mgombea wa CHADEMA, Elishadai Ngowi amemshinda mgombea wa CCM, Edina Sauli kwa kura 2,265, dhidi ya 1,169 za mpinzani wake.

Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jiji la Arusha lilizizima kwa shangwe na nderemo, huku idadi kubwa ya watu wakijipongeza kwa ushindi huo mkubwa.

Mwigulu Nchemba atimua

Matokeo hayo ambayo yameonekana kuwasononesha viongozi na wanachama wa CCM, yalimfanya Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba, kuondoka kimya kimya jijini hapa kwa kutumia gari maalumu.

Mwigulu ambaye aliongoza kikosi cha CCM katika kampeni za kimya kimya, majira ya jioni alionekana akielekea Moshi, huku wasaidizi wake wakiwemo wabunge wakitoweka katika vituo vya kuhesabia kura.

Mapema, wabunge wa CHADEMA na wa CCM tangu asubuhi walikuwa wakizunguka katika kata hizo, huku Mbunge wa Viti Maalumu, Catherin Mgige (CCM) akitumia gari ndogo, Salon yenye vioo vya giza alionekana akizunguka kata zote jana.

Ulinzi mkali wa polisi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatusi Sabas jana aliongoza kazi ya ulinzi uliokuwa na idadi kubwa ya askari polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi.

Akitumia gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba TP 1715, Kamanda Sabas alionekana akizunguka katika mitaa ya kata zote nne, zilizokuwa zimesheheni idadi kubwa ya askari, wengi kutoka mkoani Kilimanjaro.

Waangalizi wa kimataifa

Katika tukio la kwanza la kihistoria, uchaguzi wa kata hizo ulishuhudiwa na waangalizi wa kimataifa kutoka taasisi ya International Low and Policy Institute yenye makao makuu yake nchini Norway, na wale wa ndani kutoka Jukwaa la Katiba.

Kiongozi wa waangalizi kutoka Norway, Sterling Roop, akiongea na Tanzania Daima alisema kuwa idadi ndogo ya wapiga kura imejitokeza na uwepo wa dosari kadhaa umewafanya baadhi ya wananchi kukosa haki yao ya kupiga kura.

Roop alisema pamoja na wananchi kuwa na shahada halali za kupigia kura na majina yao kuwepo, lakini hakukuwa na picha zao katika daftari la wapiga kura na hivyo wakazuiwa kupiga kura.

Katika vituo vingi, hususani Kata ya Kaloleni dosari kuu ilikuwa ni kukosekana kwa majina katika daftari la kupiga kura kwa wananchi ambao wana shahada na pia majina yao kubandikwa katika ofisi za kata kama wapiga kura halali.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO