Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Simulizi ya Julius Mtatito kutoka Mtwara - JWTZ wanatumika vibaya na CCM....


Mtatiro
 
“JWTZ wanatumika vibaya na CCM....

Eti jana wamekuja na magari yao kwenye
hoteli niliyofikia mara tatu.
Mara ya kwanza wamefika wanamuuliza
muuza duka aliye karibu na hoteli kuwa ati
kama nipo hotelini, akawaambia wawaulize
wenye hoteli, wakasepa.
Baadaye saa 1 jioni wamerudi na magari
mawili, moja likapitiliza na lingine
likamshusha ofisa aliyevaa kiraia, wakati
anashushwa mita 100 kutoka hotelini kwa
kificho, bahati nzuri nyuma yake palikuwa
na BG wetu, akanipigia simu. Nikaona hawa
washenzi lazima tuwaeleze ukweli.
Nikafungua mlango ili nisikie ikiwa mgeni
atagonga kengele ya mlango wa reception,
kweli ikalia, mimi nikatoka chumbani moja
kwa moja, nikasema liwalo na liwe.
Nikamkabili akiwa mapokezi,
nikamuuliza.....bila shaka unamtafuta
Mtatiro, akashtuka sana, nikavua kofia,
nikamwambia ndo mimi.
Ni kama nilimpa pigo zito, akaniuliza za
siku, nikamjibu za siku kwani mara ya
mwisho tulionana lini? Akasema tulisoma
wote chuo kikuu, nikahamisha
mazungumzo, nikamwambia Mbona
mmepaki gari mbali hivyo....akache
kacheka. Nikamwambia usicheke, karibu
chumbani kwangu upaone ili mtakapokuja
kunifuata msipate shida. Akakaa kimya na
kuguna.
Nikamwambia....sitahama hoteli hii ili
kuwakimbia, nyinyi wauaji, nyinyi siyo
mungu, mnaweza kudhuru miili tu lakini si
roho na siku zenu zinahesabika, mnatumika
vibaya, mnatesa raia badala ya
kuwalinda......
Nikakasirika nikarudi chumbani. Nasikia
alibaki pale kwa dakika 3, akaomba kiberiti
kwa mhudumu ili avute sigara, mhudumu
akamwambia pale aliposimama sigara
haziruhusiwi.
Walinzi wetu walishafika, akawapigia simu
wenzake, gari yao ya jeshi ikasogea
hotelini. Akatoka, wakaondoka.
Dawa ya hawa washenzi si kuwakimbia, ni
kula nao sahani moja tu. Kama wao
wameshapewa kibali cha "piga tu" nasi
lazima tujichunge. Na jana niliapa,
wangeniletea ushenzi, kabla hawajaniua,
ningemwaga ubongo wa mmoja wao ili
niache kumbukumbu. Hatuwezi kuishi
katika nchi yetu kama wakimbizi.
Hatuwezi kuacha raia wateswe na
kunyanyaswa eti viongozi tunaogopa kufa.
KIFO kipo tu, hata Mahita alistaafu na siku
moja atakufa”

Maelezo haya yanatoka katika ukurasa wa facebook wa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Ndg Julius Mtatori

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO