Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MWANAMAMA ANAYEDAIWA KUTAKA KUMUUA MUMEWE AFIKISHWA MAHAKAMANI ARUSHA

MWANAMKE anayedaiwa kupanga njama za kumuua mumewe wa ndoa na mtoto wamumewe, jana amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Arumeru, iliopo Sekei, akiwa na mtuhumiwa mwingine wa mauaji hayo.

Watuhumiwa hao ni Janeth Jackson (32),mkazi wa Moshono jijini Arusha
na Novatus Elias, walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha /Arumeru, Devotha Kamuzora na
kusomewa makosa mawili ya kula njama ya kutaka kumwua Simon Jackson
ambaye ndiye mume wa Janeth.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali,Edna Kasala alidai mahakamani hapo
kuwa, washitakiwa wote wawili, walitenda kosa la pili ya kula njama na
kutaka mumuua Desderi Sabas, ambaye ni mtoto wa nje wa mume huyo
anayeishi Bukoba mkoani Kagera.

Washitakiwa  wote hawakutakiwa kujibu lolote mahakamani hapo, kwa
sababu Mahakama hiyo kisheria haina mamlaka ya kusikiliza kesi za
mauaji.

Mwendesha Mashitaka huyo wa serikali iliiomba mahakama kuwanyima
dhamana, watuhumiwa kwa sababu watuhumiwa wengine wawili katika kesi
hiyo bado wanatafutwa na hivyo kuwapa dhamana, kunaweza kuharibu
upelelezi ambao bado haujakamilika na washitakiwa hao wakatokomea
kusikojulikana.

Alisema kutokana na uzito wa tuhuma hizo, maombi hayo ya kuwanyima
dhamana watuhumiwa yameambatana na hati ya kiapo ya Mkuu wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha, akisisitiza kutowapa dhamana, licha
ya makosa hayo kuwa na dhamana.

“Mheshimiwa tunafahamu kwamba dhamana ni haki ya kikatiba ya kila
mtu,lakini kutokanana mazingira ya kesi hii kuwa magumu tunaomba
dhamana isitolewe, ili kuwatafuta watuhumiwa wengine wa kesi hii, na
hawa wasikimbie pia,’alisema MwendaMashitaka huyo.

Kwa upande wake,Wakili wa Utetezi,Fidelis Peter alipinga maombi hayo
na kutaka mahakama itoe dhamana kwa washtakiwa, kwa sababu ni haki yao
ya kikatiba na kuwa hilo lilikuwa kosa lao la kwanza.

Alitoa sababu nyingine ya kupinga maombi ya upande wa mashitaka kwamba
sababu kuwa watuhumiwa wanaweza kuvuruga upepelezi akiachiwa, kuwa si
za msingi kwa ni watu wanaoaminika katika jamii.

“Mheshimiwa sababu za kuwanyima dhamana watuhumiwa hazina uzito wowote
pia mshitakiwa wa kwanza(Janeth) ana mtoto wa miezi sita na tangu
akamatwe alhamisi iliyopita hajamwona wala kumnyonyesha mwanaye  hivyo
anastahili kupewa dhamana,”alisema Wakili Peter.

Hata hivyo,baada ya kusikiliza maombi ya pande zote mbili. Hakimu
Kamuzora alikubaliana na maombi ya upande wa mashitaka na kuamuru
watuhumiwa warejeshwe ndani, hadi Agosti 5,mwaka huu,kesi hiyo
itakapotajwa tena.

“Kutokana na uzito wa kesi hii, nakubaliana na hati ya kiapo ya Mkuu
wa Upelelezi ya kutowapa dhamana hadi hapo itakapobidi kufanya hivyo,
hivyo naomba mshitakiwa awe chini ya ulinzi,”alisema kamuora.

Katika kesi hiyo iliyovuta hisia watu wengi jijini hapa,inadaiwa kuwa
Janeth alitaka kumwua mumewe ambaye ni mfanyabiashara ya madini
Ya tanzanite na mwanaye wa kiume ili arithi mali na utajiri alionao
mfanyabiashara huyo.

Akiwa amejifunika uso muda wote alipokuwa mahakamani, Janeth
alionekana kuwa na mawazo mengi na macho mekundu kwa sababu ya kulia
baada ya njama hizo kugonga mwamba

Hata hivyo nje ya Mahakama hiyo, habari za uhakika zilizopatikana
kutoka ndani ya familia hiyo, zimedai mshitakiwa huyo ana watoto
wawili ambao, mmoja ana miaka mitatu na mdogo ana miezi tisa na siyo sita kama alivyodai Wakili wa utetezi.

TAARIFA YA AWALI YA POLISI

JESHI la Polisi jijini hapa limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja kati ya wawili waliyedaiwa kuagizwa na Janeth Jackson kufanya mauaji ya mume wake ambae ni Mfanyabiashara wa madini jijini hapa Jackson Kaijage pamoja na mtoto wake wa kiume aliyezaa na mfanyabiashara huyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa jiji la Arusha, Liberatus Sabas, mtuhumiwa huyo Novatus Elias Mrisha(35) alikamatwa na makachero wa jeshi hilo katika mji wa Bukoba Mkoani Kagera akiwa katika hatua za mwisho za kutekeleza mauaji hayo huku mtuhumiwa mwingine akitoroka.

Kamanda Sabas alisema kuwa baada ya jeshi hilo la polisi kupata taarifa ya uwepo wa mpango wa mauaji hayo, Julai 17 mwaka huu jeshi hilo lilituma makachero wake Bukoba kufuatilia wauaji hao na kuwanasa.

Alisema makachero hao walifika Julai 18 mwaka huu na ilipotimu saa 4.00 usiku wauaji wakiwa katika harakati za mwisho za kutekeleza mauaji kwa mtoto huyo wa kiume wa Jackson anayeishi mjini humo walifanikiwa kumnasa mtuhumiwa mmoja aliyetajwa kwa jina la Novatus Elias Mrisha (35).

“ Julai 18 mwaka huu saa 4.00 usiku kikosi cha askari waliotumwa kutoka Arusha kwa kushirikiana na askari Polisi Mkoani Kagera waliweza kumkamata mtuhumiwa mmojawapo kati ya watuhumiwa wawili waliokuwa wamekwenda Bukoba kutekeleza mpango wa mauaji ambapo mtuhumiwa Novatus mkazi wa moshono alikamatwa na mtuhumiwa mwingine alifanikiwa kutoroka,”alisema Sabas.

Kamanda Sabas alisema kuwa mpango huo wa mauaji ulipangwa kufanyika  katika miji ya Bukoba kwa wauaji kumuua mtoto wa mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 12 pamoja na ndugu zake kadhaa na baadae kumalizia mpango huo wa mauaji kwa kumuua mume wake Jackson Kaijage
maarufu kwa jina la ‘Jackson Manjuruu’ jijini Arusha.

Kamanda Sabas alisema baada ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na kuhojiwa alikiri kuhusishwa katika mpango huo wa mauaji na kumtaja mke wa mfanyabiashara huyo kuwa ndiye aliyewatuma kwenda kutekeleza mpango huo.

“Mke wa mfanyabiashara huyo aitwaye Janeth Jackson (32), mkazi wa Moshono amekamatwa na anaendelea kuhojiwa, watuhumiwa wote hao wawili watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika,”alisema Kamanda Sabas.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zilidai kuwa Janeth Jackson alipanga kumuua mumewe huyo kwa lengo la kurithi mali walizokuwa nazo ikiwa ni pamoja na kuwaua mtoto wake na ndugu zake wa karibu .

Wakati huo huo, Kamanda Sabas alisema kwa jeshi hilo limekamata dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilo 50 zilizokuwa zikisafirishwa na gari aina ya Nissan Mingroad namba za usajili
T904 BSJ kutokea eneo la Unga limited kuingia katikati ya mji.

Sabas alisema kuwa jeshi hilo lilipata taarifa ya kubebwa mirungi ndani ya gari hilo na kuweka mtego ili kuwanasa watuhumiwa lakini hata hivyo walifanikiwa kukamata dawa hizo pekee kufuatia watuhumiwa waliokuwa wakiendesha gari hilo kulitelekeza gari na kukimbia kusikojulikana.

CHANZO: PAMELA MOLLEL

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO