Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Hatima makada wa Chadema walioko Tabora kujulikana leo

 

Hatima ya makada watano wa Chadema, wanaokabiliwa na kesi ya ugaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora, inatarajiwa kujulikana leo, wakati mahakama hiyo itakapotoa uamuzi kuhusiana na kesi hiyopamoja na mambo mengine, uhalali wa mashtaka yanayowakabili.

Makada hao wa Chadema, Henry John Kilewo, ambaye ni Katibu wa Chadema Wilaya ya Kinondoni,  Evodius Justinian, Oscar Kaijage,  Rajabu Daniel, Seif Magesa Kabuta, walipandishwa kizimbani mahakamani hapo na kusomewa mashtaka mawili, moja la ugaidi na lingine la jinai.

Katika shtaka la kwanza wanashtakiwa chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi, wakidaiwa kumteka kwa nia ya ugaidi Mussa Tesha huko Igunga, Tabora,  na la pili wanashtakiwa chini ya Sheria ya Kanuni za Adhabu wakidaiwa kumdhuru Tesha kwa kumwagia tindikali.

Walidaiwa kutenda makosa hayo mwaka 2011, wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mawakili wao, Peter Kibatala na Profesa Abdallah Safari walipambana kuwanusuru na mashtaka hayo.

Mawakili hao walihoji uhalali wa mashtaka hayo,wakidai kuwa hakuna vigezo vya kutosha kuonyesha kuwa kuna ugaidi, huku pia wakihoji utaratibu wa kuwafungulia mashtaka katika mahakama hiyo badala ya kule walikokamatiwa.

Hivyo waliiomba Mahakama hiyo ama iwafutie mashtaka hayo au iamuru kila mshtakiwa arudishwe na kushtakiwa katika mahakama za mahali walikokamatiwa.

Upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Juma Masanja akisaidiana na Wakili wa Serikali, Idelfonce Mukandara, walidai mashtaka hayo ni halali.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Joctan Rushwera aliahirisha kesi hiyo na kupanga kutoa uamuzi leo.

Hakimu Rushwera aliamuru washtakiwa wote wapelekwe mahabusu wakisubiri uamuzi wa kesi yao leo, kwa kuwa mashtaka yanayowakabili hayana dhamana.


KWA MUJIBU WA MSEMAJI WA CHADEMA, TUMAINI MAKENE

Mwanzoni washitakiwa wanne ukimtoa Henry Kileo walikuwa wameshitakiwa Igunga kwa shitaka la kushambulia na kudhuru mwili katika Mahakama ya Igunga, wakaachiwa kwa dhamana na kisha kukamatwa tena na kupelekwa Tabora.

Leo Mahakama itatoa uamuzi juu ya hoja za upande wa utetezi unaoongozwa na Mawakili Profesa Safari na Peter Kibatala, ambazo zilikuwa ni kufuta kesi ya ugaidi kwa sababu
1. Hakukuwa na consent ya DPP kama sheria inavyosema na upande wa mashitaka umefungua kesi bila kufanya hivyo.

2. Kuna kifungu cha sheria kinaeleza kuwa kila mshitakiwa ashitakiwe alikokamatwa, na

3. Maelezo ya mashtaka hayaoneshi huo ugaidi kiasi cha kutofautisha na makosa mengine ya kijamii, ambayo wangeshitakiwa na kupata dhamana.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO