Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

HENRY KILEWO NA WENZAKE WAZUIWA KUVAA MAGWANDA YA CHADEMA NA UONGOZI WA GEREZA

 
“Jana nilikuwa mkoani Tabora nilikoenda kumsalimia kamanda Kileo na watuhumiwa wenzake wanaoshtakiwa kwa makosa ya ugaidi ya kummwagia tindikali Musa Tesha kipindi cha uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga.

Lakini baada ya kuingia na kuonana na kamanda kileo nilipata mshtuko baada ya yeye kuniambia kuwa amezuiliwa kuvaa magwanda ambayo wanapenda kuyatumia CHADEMA na kutakiwa kuvaa nguo za kawaida.

Kileo alienda mbali zaidi pale aliposema kuwa hata nguo alizompelekea mke wake ambazo zilikuwa ni magwanda viongozi wa prison walizichukua na kumwambia kuwa atazivaa siku ya kwenda mahakamani,

Pia nikajaribu kufuatilia kuwa limeishia wapi ndipo nikapewa taarifa kuwa kuna mwanasheria mmoja(jina linahifadhiwa) toka hapa mkoani-Tabora alilifutilia suala hilo na kuambiwa kuwa viongozi wa magereza ya Uyui walipewa maelekezo toka kwa viongozi wa juu.

Pia akasema kuwa serikali inafanya hivo ili kupunguza nguvu ya CHADEMA ndani ya magereza kwani watu huishabikia sana.

Mungu tulinde na uipe mahakama nguvu”

Chanzo: ManAlony

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO