Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Mkanda mzima jinsi Polisi walivyohangaika na Joshua Nassari tokea JKIA hadi nyumbani kwake...

HATUA KWA HATUA SAFARI YA NASSARI TOKA DAR NA MIZINGUO YA JESHI LA POLISI HADI HOME KWAKE
1. Jana Julai 10, 2013 Mbumge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) alirudi Jimboni kwake tokea Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa
matibabu kufuatia kipigo alichopata wakati wa uchaguzi wa diwani Kata ya Makuyuni.
2. Ratiba ya kurejea kwake ilihusiha mapokezi ya ndugu, jamaa, marafiki na watu wa Chadema kuanzia uwanja wa mdogo wandege Arusha na baadae kufanya mkutano wa hadhara Jimboni kwake eneo la Liganga - Usa River.
3. Bahati mbaya raiba hiyo haikuweza kukamilika baada ya Jeshi la Polisi luweka zuio la kutokuwako mkutano wana shamrashamra za mapokezi kwa mtu yeyete kwasababu za kuwako kwa chaguzi za udiwani Arusha Mjini keshokutwa Jumapili Julai 14, 2013.
4. Maandalizi ya zuio la Jeshi la Polisi yalianza asubuhi kwa kuweka utepe kuzunguka eneo walilotenga katika uwanja wa ndege Arusha na skari wenye silaha wakilinda na pia kusambaza gari la majii ya kuwasha na askari wengi kulinda viwanja vya wazi Usa River wakiwa na mabomu, bunduki, mbwa na farasi.
5. Kwa kiasi kikubwa zuio hilo la Polisi lilipokelewa vyema na maelfu ya watu wa Chadema waliokuwa wameshajpanga kwa wingi kumpokea Mbunge Nassari na kuhudhuria mkutano wake wa Arumeru Mashariki.
6. Mh Nassari aliwasili uwanja wa ndege Arusha majira ya mchana na kupokelewa na watu walionea gari mbili tu zilizoruhusiwa na Jeshi la Polisi, saloon moja na Jeep ya wazi iliyombeba nassari.
7. Msafara wa gari hizo mbili za Nassari ulisindikizwa kwa ulinzi mkali na magari (Landcruiser) za Jeshi la Polisi kwa nyuma na mbele zikiwa zimesheheni askari wenye silaha kali hadi ofisi kuu za Chadema zilizopo Ngarenaro Arusha. Nassari akaingia ofisini askari wakapaki pembeni kuendelea kulinda walichoagizwa kulinda.
8. Njiani kulikuwa na wananchi baadhi wenye magari na bodaboda waliotaka kuunga msafara lakini kabali ya Polisi iliwafanya wasiweze kuunga msafara huo.
9. Katika ofisi za Chadema walikuwepo wanachama kiasi na viongozi wa Chama ngazi ya Mkoa na Kanda, sambamba na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Lema na waandishi wa habari, wote wakimsubiri Nassari wampokelee ofisini hapo baada ya kuzuiwa uwanja wa ndege. Pia walikuwapo wagombea udiwani wa Kata za Kaloleni na Elerai ambao walitangazwa na watu wa CCM kuwa wamejitoa ili kuwahadaa.
Press Conference
10. Mh Nassari aliongea na waandishi wa habari ofisini hapo na kueleza kwa ufupi maumivu yake na kipigo alichopata na kudai kuwa aliumia zaidi uti wa mgongo.
11. Nassari akasema kwa sasa yuko salama na mzima wa faya na atashiriki kwa ukamilifu katika chaguzi za udiwani na ataongoza kikosi maalumu kwa Kata mojawapo kulinda kura za Chadema isiibiwe hata moja kama sheria zinavyoagiza ili haki itendeke.
12. Nassari alishangazwa na kulaani uamuzi wa Jeshi la Polisi kumfuatiliatangia uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na kisha kumzuia kabisa asionane na watu wake ilhali wanajua Arumeru kwake ni Mamlaka tofauti na Arusha Mjini na yeye ni mbunge wa kuchaguliwa na watu hao na ametoka katika matibabu.
13. Baadae Mbunge wa Arusha Mjini akapewa nafasi ya kuzungumza na kuanika bayana mtego waliokuwa wameemtegea Mwigulu Nchemba kwa kili kilichoelezwa mnamo Juni 12, 2013 alifanya mpango wa kumrubuni mgombea wa Chadema Kata ya Elerai, Eng Mpinga kujitoa kwa kumdanganya kuwa yeye Mwigulu alikuwa ametumwa na Rais Kikwete na kwamba angekubali angepewa Ukuu wa Wilaya au cheo chochote ambacho angetaka. Lema anasema mtego huo ni kama Mwigulu aliushitukia na kwamba kama angeingia kwenye 18 angefanywa kitu mbaya.
14. Lema aksema Chadema kama chadema wanarudisha Kata zote nne na wamejipanga kwa kila hila kuhakkisha hakuna dhuluma itakayofanikiwa, ikiwemo zoezi alilodai linafanywa na maofisa wa Tume ya Uchaguzi walioko Jijini Arusha kujaribu kubadilisha majina ya daftari la wapiga kura.
15. Mh Lema alitanabaisha kuwa nae ataongoza kiksoi maalumu kwa usalama wa kura za chadema kwa Kata mojawapo na kwamba kuna baadhi ya wabunge wa Chadema watakuja Arusha kuapishwa kama mawakala na watashiriki uchaguzi huo kuhakikisha hakuna haki yao itakayodhulumiwa. Pia makamanda wao waliokuwa mikoani kama Ally Banaga na Alphonce Mawazo na wengine watarudi kuungana na wengine kuongeza nguvu ya ulinzi.Watakaofanya vurugu wapewe kichapo
16. Lema akatahadharisha kuwa kuna watu wameandaliwa kufanya vurugu wakivalishwa alama za Chadema ili ionekane ni Chadema. Lema akasema yeyote atakaefanya vurugu sio mtu wa Chadema na atashushiwa kipigo bila kujali amevaa magwanda ama kitu gani na kwamba watu wa Chadema watatambua na alama wanazozijua siku hiyo. Amewataka watu wote wa Chadema kuwa wapole lakini jasiri ili wasiwape mwanya CCM kutimiza hila zao.
Eng Mpinga akanusha kuhamia CCM, amdharau Mwigulu Nchemba
17. Mgombea wa Chadema Kata ya Elerai, Eng Jeremiah Mpinga akajitokeza mbele ya kamera za waandishi wa habari na kukanusha propaganda za Mwigulu Nchemba akimtumia kijana aliyefukuzwa Chadema, Mtela Mwampamba kupitia mitandao ya kijamii (facebook na Jamii Forum) wakidai yeye Mpinga amkubaliana nao kuhamia CCM.Eng Mpinga akasema amemdharau sana Mwigulu Nchemba na akasema hakuwahi dhani ni mpuuzi kiasi hicho kwasababu Mwigulu aliomba kuonana ane Mpinga mapema mwezi Juni, kwanza kwa kupitia viongozi wa Wilaya Arusha na baadae mawasiliano yalivyoendelea ndipo Mwigulu mwenyewe akajitokeza kwa namba yake 0714 008888 kuomba waonane akidai ana maagizo ya Kikwete.
Mzee Mpinga akasema Mwigulu ni kama ndugu yake kwasababu wanatoka maeneo jirani huko Singida na wanafahamiana. Alipomuomba kuonana nae alimkubalia kama ndugu na alikataa kukutana maeneo mengine zaidi ya nyumbani kwake.
Eng Mpinga akatanabaisha kuwa japo aliona ngumu kwenda nyumbani kwake, alilazimika kufika siku ya Juni 12, 2013 akiwa ameambatana na Mtela Mwampamba. Mzee Mpinga kwa kujihami kiusalama alibaki sebuleni kwake na red brigade mmoja na alikuwa nae sebuleni. Mwigulu alipofika akahoji huyo ni nani na kutaka aondolewe aliambiwa na mtoto wa familia na hapo ni kwake ahawezi kuondoka.
Ndipo Mwigulu Nchemba akaanza kubembeeza kwa hadaa kwamba ametumwa na Rais Kikwete kumuomba Eng Mpinga ajitoe Chadema na atapatiwa cheo au kazi yeyeote ikiwemo ukuu wa Wilaya.Mzee Mpinga akamchomolea Mwigulu katakata na Mwigulu akaondoka na kusema "Kaa ujifikirie, ukipata jibu nijulishe... Sisi (CCM) ndio tuna Serikali tunaweza kufanya chochote..)
Picha iliyowekwa Facebook na mtumishi wa Mwigulu ilipigwa kwa siri kwasababu Eng Mpinga anasema hakukuwa na tukio la wazi la kupiga picha.
Katibu wa Kanda awashukia Polisi
18. Nae Katibu wa Kanda ya Kaskazini Chadema, Mh Amani Golugwa amelitaka Jeshi la Polisi kutumia kiherehere kile kile walichokitumia kumkamata Mh Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kile alichoandika Facebook kuwa waziri mkuu ni -------- kuagiza wananchi wapigwe tu, basi wa wamkamate pia aliyesambaza picha na maelezo ya uongo huko Facebook na Jmii Forums kuwa mgombea wa Chadema amejitoa ilhali wanajua kampeni zimepigwa marufuku na Tume na taarifa yake sio ya kweli..
Safari ya Nassari kuelekea Arumeru
19. Baada ya kikao na waandishi wa habari Nassari na msafara wake wa gari mbili walondoka ofisini hapo kuelekea Arumeru. Defenda za Polisi zikawaunganishia tena kukaba msafara. Ilikuwa ni kama vile gaidi osama analindwa asitoroke.
20. Msafara ulikatiza Kilombero, Desemba, Seliani na hadi unafika mataa ya Mianzini tayari kundi kubwa la magari, boda boda n.k waliunga msafara na Polisi wasijue la kufanya. Wananchi waliokuwa pembezoni mwa barabara walishangilia sana kwa miluzi na makelele kila mahali Nassari alikopita pamoja na kukabwa na askari polisi.
21. Baadhi ya magari binafsi yaliyounga msafara kilazima yalianza kujiachia mojamojakuanzia Philips yakabaki magari kama manne hivi ambayo yalikuwa ni kutoka Arumeru. Polisi nao wakiwa nyuma, msafara ukikimbia nao wanakimbia..
22. Gari ya Polisi kutoka Arusha ilipokelewa na gari nyingine iliyokuwa imejiandaa kwa kazi hiyo, ya Arusha ikaishia maeneo ya Tengeru.
23. Maeneo ya Makumira kulikuwa na gari jingine landcruiser lenye askari walio tayari kwa mapambano na mabomu yao wametega mahali pembeni ya njia.
24. Nassari na watu wake wakafika Leganga Usa River na kushukia njia ya vumbi kulia kufuata ilikokuwa gari ya matangazo ya Chadema maeneo ya Ngaresero iliyokuwa ikiwatangazia watu kuwa mkutano wake umeahiriswa hadi watakapotangaziwa tena.
25. Hapo Leganga askari Polisi walikuwa wameziba kabisa njia inayoingia uwanja wa Shule ya Msingi Leganga, baada ya kuona Nassari ameingia njia ya vumbi nao wakaunganishia kwa nyuma kumfuata.. Baade kidogo landcruiser 2 zilizosheheni askari na silaha zao wakaunga msafara tena kumfukuzia Nassari.
26. Askari wengine kwenye Landcruiser na silaha waliziba njia ya kuingilia uwanja mwingine wa Ngarasero pale Usa River, wananchi wakiwa wametanda barabarani washangaa..
27. Nassari akiwa kwenye gari ya wazi alikutana na barrier ya Polisi baada ya kuvuka daraja Fulani kama mita 150 hivi kabla ya kuingia Usa River halisi kupitia Old Moshi road (sasa Mandela Road). Barrier hii iliongozwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Usa River ..kama sijakosea ni Mussa Sindi Huya
28. Kufikia hapo hali ilianza kuwa mbaya, Polisi walikomaa Nassari waondoke nae bila mtu mwingine yeyote. Nassari nae hataki. Mabishano yakawa makali sana kiasi cha askari wote kushuka kwenye magari yao na kuwazingia Chadema huku silaha zao zikiwa tayari tayari kwa lolote. Punde kidogo gari 2nyingine 2 za Polisi zikaongezeka na kupaki mwanzo wa daraja, Nassari na Chadema wake wakawa wamewekwa Kati huku mabishano yanaendelea. Watu wa Chadema waliokuwa nje ya magari ni reed brigade peke waliokuwa kwenye gari ya wazi..wengine walikuwa ndani ya magari yao kama matatu wakisubiri hatma ya hali ile.
29. Wakati Mkuu wa Kituo yuko bize kuwasiliana na Nassari nae alikuwa busy pia kuwasiliana na wote wakimaliza kila mmoja anadai ameelekezwa hivi na ndicho kilicho sahihi. Kiongozi huyo wa Polisi alionekana kama anapokea maagizo fulani kila anapoambiwa taarifa mpya na Nassari kutoka mahali Fulani..
30. Nassari akawaambia kama ni vipi aende mwenyewe kwa mguu hadi Ofisini kwake na hao wenzake warudi. Polisi wakakataa, wanataka waondoke nae wao.
31. Baada ya mzozo kutokuwa na muafaka na dalili ya hali kuchafuka zaidi, magari yote yaliamriwa kugeuza kurudi yalikotoka. Madereva wakatii na kugeuza lakini kusogelea darajani wakakuta gari za Polisi zimeziba, wao wako kati na dalili ya Polisi kukinukisha iko wazi..
32. Nassari akapanda boda boda na kuondoka eneo hilo, hatua hiyo ikawalazimu Polisi kuwasha landcruiser zao na kuanza kumfukuzia na hapo kutoa mwanya kwa gari zilizokuwa ziimewekwa kati kugeuza tena kwa kasi ya ajabu na kupenya huku nyingine zikikatiza kwenye mahindi ya watu na kutimka lakini wakakutana na kizuizi kingine cha Polisi inapotokea Mandela road kuunga na barabara kuu ya Moshi Arusha.
33. Nassari alifika mahali huku anafukuzziwa na askari Polisi akaacha ile bodaboda akaingia kwenye Suzuki iliyokuwa na Katibu wake, Toti Ndonde akiwa na watu wengine wawili. Wale watu wengine walishatawanyika kila mtu na njia yake.
34. Askari Polisi waliendelea kuifukuzia Suzuki hiyo hadi ikafikia mahali Nassari akashuka na kuwaluliza wanamfuatilia nini hivyo? Askari wale wakajibu yeye aendelee na shuguli zake wao wanayao. Nassari akarudi garini safari ikaendelea. Sasa alikuwa anaelekea shambani kwake anakojenga nyumba yake. Polisi bado wanamfukuzia.
35. Nassari akafika restaurant fulani akaamua kushuka kwenye gari aende chooni kujisaidia, Polisi bado wamekaba.
36. Nassari akaenda hadi kwenye nyumba yake anayojenga, akakagua mambomambo hapo.. Polisi bado wamekaba na landcruiser lao. Kha!
37. Baada ya kutoka maendeleo ya kazi ya ujenzi na kuona hali ya kufuatwa inaendelea, ikabidi dereva akaimbize gari na kuwapotezea vichochoroni.HII NDIO KAZI YA JESHI LA POLISI KWA SASA… WAKATI WAHALIFU WANAKULA RAHA WAO WANAHANGAIKA NA WATU WEMA TENA VIONGOZI WAKUBWA KABISA!!

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO