Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Kunisaga (DC. Nyamagana) akimpokea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa (MB-Monduli) alipowasili uwanja wa ndege wa Mwanza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza (RAS) Doroth Mwanyika akisalimiana na Mhe.Lowassa baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwanza anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mery Tesha
Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Lowassa akisalimiana na Shekh Ferej ambaye aliongoza mashekh na viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza uwanjani hapo kumpokea.
Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza Shekh Mohamed Bara akisalimiana na Waziri Mkuu msataafu Mhe. Edward lowassa uwajna wa ndege
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Seleman Mzee alikuwepo kwenye mapokezi na hapa akisalimiana na Mhe. Lowassa
Kada maarufu wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wa Wilaya ya Busega Dkt. Raphael Chegeni akisalimiana na Mhe. Lowassa
Mh Edward Lowassa akiwa ameambatana na makada wa chama, wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa wamachinga wa jijini Mwanza, wakitembea kuelekea eneo la Makoroboi kwaajili ya mkutano wa muda mfupi ambapo kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Monduli alikutana na wamachinga wa jijini hapa.
Alipowasili alikaribishwa kishupavu na vijana.
Kisha akapanda mti eneo hilo ikiwa ni ishara ya kuthamini mazingira.
Naye diwani wa Nyamagana Bhiku Kotecha alifungua mkutano huo kwa maneno machache.
Wananchi kusanyikoni.
Jiografia ya eneo la Makoroboi jijini Mwanza na umati wake.
Mhe. Lowassa akisalimiana na mmoja kati ya wachezaji wadogo kuliko wote wa timu ya Machinga Fc inayoshiriki ligi ya kuwania kombe la Meya's Cup jijini Mwanza.
Timu ya Machinga inayoshiriki ligi ya Meya's Cup nayo ilitambulishwa.
Lowassa akiwapa somo wamachinga Mwanza.
Maneno yaliyowagusa.
“Ninyi ni watanzania wenye kujiamini na kujitafutia ridhiki kwa kufanya biashara zenu kwewnye Taifa lenu mkiwa huru na amani, lakini mkiwa hamna mijati hamtaweza kufika pahali popote hivyo niwaombeni sana wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwachangia ili kuwawezesha kupata mtaji wa kuwaendeleza na kujiingizia kipato katika biashara zenu za ujasiliamali”alisema.
Makoroboi jijini Mwanza.
Mhe. Lowassa akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 20 Bw.Matondo ambaye ni mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa wafanyabiashara wadogowadogo wa jijini Mwanza (SHIUMA) huku akishuhudiwa na diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha (anayepiga makofi).
Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Edward Lowassa akizungumza na wananchi waliojitokeza katika hafla ya Harambee iliyofanyika katika Hotel Gold Crest jijini Mwanza, kuwahamasisha kutambua nini wanapaswa kufanya ili kufanikisha lengo lililokusudiwa.
WAZIRI Mkuu wa zamani aliyekiuzulu kufuatia skendo ya Richmond Mhe.Edward Lowassa ijumaa usiku aliongoza harambee kubwa na ya kihistoria ya kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm kinachomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.
Mhe.Lowassa aliyekuwa Jijini Mwanza kushirikiana na marafiki zake, wafanyabiashara, taasisi na makampuni mbalimbali, watu binafisi na viongozi wa serikali na vyama vya siasa na wabunge wa majimbo mawili ya jijini Mwanza Ilemela na Nyamagana kupitia CHADEMA yaliyotuma wawakilishi wao hatimaye aliweza kuvuka lengo lililowekwa kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 590 zikiwemo ahadi.
Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza ambaye pia ni Mzee wa baraza la wazee Mwanza Mjumbe wa NEC wilaya ya Tarime Mhe. Christopher Gachuma akimkabidhi mmoja wa wazee wa kiislamu aliyeketimeza kuu kanzu pamoja na joho kama zawadi aliyovikwa mgeni rasmi Mhe. Lowassa.
Lilikuwa tukio la kipekee Mhe. Lowassa alivikwa na kukabidhiwa zawadi ya kibarakashia juu..
"Ninaamini vituo vya redio Iqra FM na redio Sauti ya Qur-ani kitaonyesha Uislamu kama dira unayohusisha mambo yahusuyo jamii. Ni cheche ya kimungu ambayo inatoa ubinafsi pia inayo waunganisha binadamu katika jamii moja. Korani inasema binadamu ameumbwa kutokana na roho moja, kama mwanaume na mwanamke, jamii na mataifa, ili watu waweze kufahamiana. Inawaleta watu wa imani zote kwenye jukwaa moja, kwa kupitia wema."
CHANGIZO LIKAANZA:
Mmoja kati ya wanakamati wa SHIUMA akionyesha hundi ya shilingi milioni 20 waliyokabidhiwa na Mhe. Lowassa kama sehemu ya harakati ya kutatua masuala mbalimbali ya changamoto zao walizoziainisha kwenye risala.
Mkutano huo wa muda mfupi ulipo malizika tu Mhe. lowassa akiwa ameambatana na wamachinga mguu kwa mguu walimsindikiza hadi hoteli aliyofikia.
Mfanyabiashara maarufu wa Mkoani Arusha na Mjumbe wa NEC (CCM-Taifa) Wilaya ya Arumeru ambaye ni mwekezaji mkubwa wa Jiji la Mwanza naye alikuwepo kumpokea
MKUSANYIKO WOTE WA MATUKIO YOTE NI KWA HISANI YA: GSENGO BLOG
0 maoni:
Post a Comment