Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kesi ya Lwakatare yaahirishwa hadi 22 Julai, 2013; Ludovick akwama tena kupata dhamana

LwakatareMkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Mh Wilfred Lwakatare akiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliporipoti asubuhi ya leo kusikiliza kesi yake. Kulia kwake ni kijana Ludovick Joseph, mshitakiwa namba mbili ambaye amekosa dhamana tena baada ya ndugu zake kutotokea kukamilisha taratibu za dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa tena mpaka Julai 22, 2013 itakaposikilizwa tena mahakamani hapo.


Kupitia mtandao wa Facebook, Lwakatare ameandika hivi..

”Nimshukuru Mungu kwa siku njema ya leo na kwa ajili ya watanzania wote. Leo ikiwa ni siku ya case yangu kusikilizwa Mahakama ya Mkazi Kisutu, nimereport pamoja na makamanda walionisindikiza. Case imehairishwa mpaka tarehe 22 July 2013.

Pamoja na hayo,mshitakiwa no.2 Ludovick Joseph ameshindwa kupata dhamana kwa sababu ya kutokukamilika kwa nyaraka za dhamana,hata hivyo dhamana yake iko wazi.

Tukiwa nje ya mahakama,kijana Ludovick ameonekana kuwa mnyonge na kulia sana akilalamika kutojishughulisha kwa ndugu zake(ambao hawakufika mahakamani) kufuatilia dhamana yake.
Nawatakia kazi njema na tusichoke kulitumikia taifa.
Peopleeeeeeeeeeees!”

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO