Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MKE WA RAIA OBAMA, MICHELLE OBAMA ATEMBELEA WAMA FOUNDATION NA KUKUTANA NA MAMA SALMA KIKWETE JIONI HII

1

Mke wa Rais wa Markani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA  jioni hii wakati alipotembelea katika ofisi hiyo na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa  WAMA Mama Salma Kikwete katika makao makuu ya taaisis hiyo leo, Rais Barack Obama na Mke wake Michelle Obama wako  katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini Tanzania wakiongozana  na watoto wao jioni hii Rais Barack Obama atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na pia watazungumza na waandishi wa habari Ikulu kabla ya kuendelea na kazi zingine.

 2

Mama Mchelle Obama akielekea katika lango kuu la ofisi za WAMA jioni hii. 3

Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi. 4

Mama Michelle Obama akipozi kwa picha na mwenyeji wake mama Salma Kikwete  6

Wake wa viongozi wakipunga bendera kama ishara ya kumpokea Mama Michelle Obama

 7 8 9

Mama Anna Mkapa ambaye pia ni mwenyekiti wa taasisi ya EPTF akiongozana na mama Aisha Bilal wakati wa mapokezi ya Mke wa Rais Barack Obama Mama Michelle Obama katika ofisi za WAMA jioni hii 10Makachero wa Marekani wakiwa kazini 11

Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wake wa Viongozi wakati alipowasili katika ofisi za WAMA tayari kwa kumpokea mgeni wake Mama Michelle Obama.

CHANZO: HENRY MDIMU BLOG


Wake wa marais kuzungumzia nafasi ya mwanamke Afrika

Wake za marais kutoka mabara mbalimbali duniani, leo wanakutana kuzungumzia majukumu muhimu ya wake za marais katika kutetea elimu, afya na uchumi wa wanawake duniani.

Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Rais wa zamani wa Marekani, George W. Bush utawakutanisha wakwe za marais, maofisa wa Serikali, taasisi binafsi na wanataaluma kujadili utendaji bora wakati wa ushirikiano wa taasisi binafsi na Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana, majadiliano hayo yatawanufaisha wanawake, kisiasa, kiafya na kiuchumi na hatimaye kujenga jamii imara.

Rais Bush na mke wake, Laura watazungumza kwenye mkutano huo ambao utahudhuriwa na mke wa Rais Barack Obama, Michelle, Salma Kikwete, Roman Tesfaye wa Ethiopia na Maria Da Luz wa Msumbiji.

Wake wengine wa marais ni Panehupifo Pohamba wa Namibia, Sia Nyama Koroma wa Sierra Leone, Janet Museveni wa Uganda na Christine Kaseba wa Zambia.

Wengine ni Cherie Blair, Mwasisi wa Mfuko wa Wanawake wa Cherie Blair na Nancy Brinker, Mwenyekiti wa Mpango wa Kupambana na Saratani. Mengine yatakayozungumzwa ni masuala ya usalama, mbinu za kupambana na saratani ya shingo ya kizazi na maziwa, elimu na kuwainua wanawake kibiashara kupitia mafunzo na teknolojia

Mwananchi

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO