Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: JINSI SIKU YA SERIKALI ZA MITAA ILIVYOFANA MANISPAA YA IRINGA

Mbunge Msigwa na  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  wakitazama  ndizi aina ya Jamaica inayolimwa Mtwivila Iringa iliyoletwa katika maonyesho ya  serikali za mitaa leo mjini Iringa

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini akiwasili jukwaa kuu na kusalimiana na mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Leticia Warioba

Hapa  mbunge Msigwa akisalimiana na naibu meya  wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki

Mtaalam kutoka AMREF Bi Stellah akitoa maelezo kuhusu huduma  zinazotolewa na AMREF

Mhandisi  wa Manispaa ya Iringa Mashaka Luhamba  akitoa maelezo ya idara ya ujenzi inavyofanya kazi katika Manispaa ya  Iringa ambao kwa sasa  wamepiga hatua katika  ukarabati wa barabara za mitaa

Maofisa  habari  wa  Halmashauri ya  manispaa ya  Iringa Sima Bingileki kushoto akiwa na msaidizi wake Janeth Matondo leo  katika maadhimisho hayo ambapo  IMTV wamepata  kupongezwa kwa  kazi nzuri  inayofanyika ya upashaji habari  mjini Iringa

Mkuu  wa wilaya ya  Iringa Dr Leticia  Warioba akimtazama  kwa makini  askari wa kikosi cha  zimamoto mjini Iringa akionyesha jinsi  ya kuzima  moto


Watangazaji  wa kituo  bora  cha matangazo  cha  televisheni ya  Manispaa ya  Iringa (IMTV) wakiwa katika banda lao la maonyesho leo katika  viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa

(Picha Zote na:  Francis Godwin  - Mzee wa Matukio  Daima)

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO