Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

“ MUNGU TUNAKUSHUKURU , ARUSHA ASANTENI SANA “– Mh Godbless Lema


Ninatafakari sana na ninaendelea kutafakari wema wa Mungu katika harakati zetu za kutafuta Uhuru wa kweli katika Taifa letu , ushindi katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika tarehe 14/7/2013 ni ushindi wa maana na muhimu sana katika Siasa za Tanzania na wala sio Arusha peke yake , Nchi nzima kuna furaha kwa watu wote wanaopenda mabadiliko na ndio maana tunasema “ MUNGU TUNAKUSHUKURU , ARUSHA ASANTENI SANA “

Ni uchaguzi uliowahi kuwa mchungu sana kwangu na watu wa Arusha na Tanzania nzima na pia ni uchaguzi uliokumbwa na mikasa na uadui mkubwa dhidi ya haki na maisha ya binadamu wa Mungu. Najua tumeshinda uchaguzi huu lakini mioyo yetu ikiwa na majeruhi na mateso makubwa dhidi ya uonevu na mateso tunayoendelea kupewa . Wakati furaha hii ya ushindi ikiwa muhimu sana kwetu na katika Siasa za Nchi yetu ni muhimu pia kuwakumbuka Ndugu , Jamaa na Watu walioumia na kupoteza maisha siku ya tarehe 15/6/2013 pale Viwanja vya Soweto baada ya bomu kupigwa kwenye mkutano wetu wa hadhara ambalo madhara yake ni makubwa zaidi katika mioyo ya Watu wote wenye ni njema na amani ya Taifa hili .
Ushindi huu tumepewa na Mungu na wala sio akili zetu na kutambua hivi ni akili na maarifa makubwa , Wengine tulipaswa kuwa tumekufa leo lakini tuko hai kwa sababu ya Mungu na hata hivyo hatujui wamepanga kutuua lini tena lakini baada ya bomu la tarehe 15/6/2013 nikiwa nyumbani usiku wa manane natafakari Mke wangu aliniambia “ Kila mahali Duniani kuna hatari , barabarani kuna ajali lakini hatuachi kuendesha magari , majumbani pia kuna hatari kwani umeme unaotumika majumbani unaweza kuwa balaa pia , kwa hiyo katika hali ya sasa ni muhimu kufikiria kupambana kwenda mbele , sisi kama familia tumeogopa na pengine ushauri wetu wa kwanza ungekuwa kukushauri uache Siasa lakini mimi nakuambia songa mbele kupigani wema na hatari zote Mungu hatawaponya Godbless , nafikiri mimi nimefanywa kuona vizuri zaidi juu ya mnachokipigania . Wanataka kuwaua ? kwanini ? nitamuomba Mungu damu za Watu waliokufa Mungu atalipa “ Usiogope Mume wangu , Mungu anakusudi lake juu ya jambo hili subiri utaona “ NEEMA LEMA .
Na Mimi nasema Tanzania Msiogope kwani giza nene linapozidi ndipo asubuhi ukaribia , mateso , dhihaka , dharau , kejeli na vipigo na mauaji ni mambo yanayoumiza mioyo yetu na yenu sana tunatembea na uchungu katika mioyo yetu lakini vumilieni bado kitambo kidogo sana Mungu ataanza mwenyewe kulipa kisasi , vumilieni tena vumilieni hakuna dola inayotesa watu wake iatakayosimama mahali popote Duniani “ Only time will tell “ wengine wanasema tuvumilie kuonewa mpaka lini ? na majibu yangu ni haya “ Mpaka Mungu atakapotoa maelekezo Mengine , Tutajuaje ? Msiogope , mtajua wakati ukifika lakini vumilieni tena mabadiliko yako karibu sana kwani Serikali inayotawala sasa ina laana na vilio na damu za watu wengi katika viganja vyake kwa hiyo hawatafika mbali sana , mtaaona na mtakuja kusema niliwaambia .

Uchaguzi huu haukuwa wa Huru na Haki hata kidogo baada ya mabomu kampeni zilizuiwa kwa Chadema takribani wiki tano lakini CCM na viongozi wake waliendelea na Kampeni za Nyumba kwa Nyumba , tulizuiwa hata kuwatangazia watu tarehe ya kupiga kura kwa kutumia magari na vipaza sauti na tume ya uchaguzi pia haikufanya hivyo kwa makini hili CCM watumie mtandao wao wa Mabalozi wa Nyumba kumi kumi kuhamasisha wanachama wao kwenda kupiga kura na Polisi pia waliendelea kutoa vitisho kwa wapiga kura hata sheria za msingi za uchaguzi zilibezwa na hakutakiwa Mtu kuonekana kituo cha kupigia kura baada ya kupiga kura vitisho hivi viliongeza hofu kwa wapiga kura na kuogopa kujitokeza huku CCM wakiamini mtandao wao wa Mabalozi ungetosha kuwapa ushindi na badala yake Mabalozi wa CCM walibeba na kukumbusha Watu kwenda kupiga kulikuwa na hila nyingi na mipango michafu mingi katika vituo vya kupigia kura , Watu walipigwa na Green Guard na polisi bila kuchukua hatua yeyote . Ndio maana tunasema “ TUNAKUSHUKURU MUNGU , ARUSHA ASANTENI SANA “
Sasa tumerudisha Viti vya Madiwani tuliowafukuza ni fundisho kwa yeyote ndani ya Chama chenu hatakayefikiri anaweza kucheza na masilahi ya UMMA na Chama chenu na Wananchi wa Arusha wamepeleka salamu nzuri sana Tanzania kwamba jina linalopendwa kuliko majina yote Tanzania ni CHADEMA na MALENGO YAKE , sio sura ya Mtu wala umaarufu wake ni MALENGO ya CHADEMA .

Arusha Mungu awabariki sana na tutaendelea kupigania haki , uhuru wa kweli , bila kuogopa matusi , kejeli , vipigo , na jela , watawatukana sana na kuwaumiza kwa njia mbali mbali kama ambavyo wengine wako magereza kwa tuhuma za uongo lakini MSIOGOPE

Tunakushukuru sana Mwenyezi Mungu na Watu wote Arusha nawapongeza kwa ujasiri wenu na uvumilivu wenu hakika kila mmoja wetu amechangia ushindi huu wale ambao hawakuweza kuwa nasi mbele zaidi walikuwa nasi kwa maombi , dua na wengine walitupa maji ya kunywa , Wazee wetu walioko majumbani pia walituombea kwa Mungu.

Timu zote za Kampeni katika kata zote wamefanya kazi ngumu bila malipo yeyote na vijana wetu wa ulinzi wameendelea kujitolea kulinda Chama na Wanchama kwa risk kubwa bila malipo yeyote kwa kweli kila mmoja wetu amekuwa muhimu kwetu hata Wapinzani wetu na Maadui zetu pia wamekuwa msaada kwani walifanya tufikirie zaidi ambayo imekuwa afya katika kupanga mikakati bora na imara zaidi .

Mwenyekiti wetu na Katibu Mkuu wetu wamefurahi sana lakini Mh Joseph Mbilinyi (Sugu ) yeye amelaumu sana kwanini CCM wamepata kura Arusha na kwa niaba yenu nimefikiria na nimeamua kumuomba Mh Joseph Mbilinyi ( Sugu ) msamaha na kuhaidi kuwa wakati unaokuja tutajirekebisha juu ya jambo hili la kuhuzunisha kwa hizo kura walizopata CCM .
Nawapenda sana Arusha , Asanteni sana .
Ni mimi Rafiki yenu .
Godbless J Lema ( MB)
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO