Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dk Vincent Mashinji hii leo ametembelea ofisi za Makao Makuu ya Jumuia ya Afrika Mashariki yaliyopo Jiji Arusha Tanzania akiambatana na baadhi ya viongozi wa chama hicho na kuweza kuzungumza na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mh Daniel Kidega na baadhi ya viongozi na watumishi wa jumuia hiyo.
Katika msafara wake Dk Mashinji ameambatana na wajumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Profesa Mwesiga Baregu na Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Tluway Sumaye pamoja na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro, ambaye pia ni Katibu wa CHADEMA Mjoa wa Arusha.
Wengine ni Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMa Mkoa wa Arusha, Mh Cecilia Pareso, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Amani Golugwa, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya Derick Magoma na Katibu wake Lewis Kopwe.
Pichani Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro (kushoto) akipokea bendera ya Jumuia ya Afrika Mashariki kutoka kwa Spika wa Bunge hilo Mh Daniel Kidega
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Vincent Mashinji na ujumbe wake katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki na maofisa wengine wa jumuia hiyo.
Dk Mashinji, Profesa Baregu na Mstahiki Meya Kalisti Lazaro wanatarajiwa kuto mada katika Kongamano la Biashara litakalofanyika katika Hotel ya News Safari ya Jijini Arusha siku ya kesho kuanzia saa 8 mchana.
Kongamano hilo la kihistoria la wasomi na wafanyabiashara litakuwa na watoa mada wahawa
1. Dr Vincent Mashinji - Katibu mkuu Wa CHADEMA
2. Mh Frederick Sumaye - Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA
3. Prof Mwesiga Baregu - Mjumbe Wa Kamati Kuu CHADEMA
4.Dr Lalitaika - Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mandela, Arusha.
PICHA ZOTE NA GODFREY STEPHEN, ARUSHA
0 maoni:
Post a Comment