Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MSTAHIKI MEYA WA KINONDONI MH BONIFACE JACOB APONGEZWA KWA KUFANIKIWA KUWAHAMISHA WAFANYABIASHARA TOKA UBUNGO MPAKA MAWASILIANO SINZA BILA MABOMU,

Meya wa Halamashauri ya Manispaa ya Kinondoni Mstahiki Meya Boniface Jacob (CHDEMA) akizungumza na wafanyabiashara wa Ubungo

Anaadika pongezi zake Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ubungo Bw Perfect Mwasiwelwa hapa chini

Prefect Mwasiwelwa
"Haijawaki kutokea wafanyabiashara watoke wenyewe Ubungo mpaka eneo lingine pasipo malumbano. Lakini kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni ameweza kufanya tukio kubwa na zito la kuwapatia wafanyabiashara maeneo ya Mawasiliano, maarufu Simu 2000.

Napenda nimpe pongezi zangu baada ya wafanyabiashara wenyewe kuelekea eneo jipya. Utawala uliopita uligawa maeneo mengi kwa madiwani...ambao kimsingi siyo wafanyabiashara...Meya kwa uungwana amenyag'anya maeneo hayo toka kwa Madiwani na kuwapatia wamachinga.

Nakumbuka miaka iliyopita kulikua na wamachinga kukimbizana na Migambo, Ubungo palikuwa hakukaliki kwa sababu ya mabomu, hali imekuwa tofauti kabisa Meya ambaye anapenda mwenyewe kuitwa Rais wa Wamachinga kuwaondoa kwa hiari yao bila hata mtu kusukumwa.

Bravo mstahiki Meya Boniface JacobManispaa ya Kinondoni hakika itazidi kuchanua"

STORI KAMILI YA KUHAMISHWA HUKO IMEANDIKWA HAPA NA MWANAHALISI ONLINE


HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imewapa wafanyabiashara wapatao 100 eneo la kufanyia biashara zao katika Soko la Mawasiliano (Sinza), anaandika Happiness Lidwino.

Kwenye soko hilo, wafanyabiashara hao hawatalipa ushuri kwa mwezi mmoja na kisha watatakiwa kulipa.

Boniphace Jacob, Meya wa Manispaa hiyo leo amesema, awali alifanya ziara katika maeneo hayo na kuzungumza na wafanyabiashara ambapo aliwataka kutofanya biashara zao kwenye eneo la Ubungo na badala yake kuhamia Mawasiliano.



“Soko hili ni kwa ajili yenu nyie wamachinga, mama lishe kila mwenye biashara aangalie kunakomfaa na kufanya biashara, kila mtu atapewa kitambulisho kutoka manispaa kimtambulishe eneo lake husika,”amesema.

Amesema, aliona si busara kuwaondoa wafanyabiashara hao bila kuwa na maeneo ya kwenda kufanya biashara zao.

“Niliomba wiki mbili kamati ya ulinzi na usalama ya kinondoni msivunjiwe hadi hapo nitakapowatafutia eneo la kufanya biashara zenu, ni jukumu langu kujua mtakwenda wapi. Kuanzia leo, atakayekuwa Ubungo asinisumbue, watu wangu wako salama mawasiliano,” amesema.

Na kwamba, hatarajii kuona Jeshi la Polisi au mgambo wanawasumbua wafanyabiashara hao huku akiwaomba kuacha njia kwa wanunuzi watakaofika sokoni hapo.


“Hakuna atakayekosa eneo la kufanyia biashara hapa, kila mtu atapata wauza mabegi ule uzio upendeze kwa kutundika mabegi na wauza nguo pia, lakini pia msilipe ushuru kwa mwezi mmoja baada ya mwezi mmoja ndiyo mtalipa,” amesema.

Meya huyo amesema, wafanyabiashara ambao tayari wamepanga biashara zao wasibugudhiwe, waliopewa na kutofanya biashara wapewe watu wengine wafanye.

Baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wakiwahi nafasi katika eneo hilo, walilalamika kwa wengine kutopata kwani tayari eneo limeonekana kuwa dogo.

Husna Khamis na Amida Juma ni miongoni mwa wafanyabiashara ambao wamesema, wana wasiwasi na maeneo hayo kutopata kwani waliowahi maeneo hayo asilimia kubwa si wafanyabiashara waliopaswa kuondoka Ubungo.

“Mimi sijapata eneo unavyoniona hapa, kila ninapoangalia naona majani watu wamewahi, ingawa Meya ametuambia tuweke biashara kama eneo halina mtu, ukienda ndani wanakuambi ulipe sh 140,000 ndiyo upate,” amesema Juma.

Awali Jacob alisema, maeneo hayo yamegaiwa bure huku akisisitiza mtu atakayeuza atachukuliwa hatua pamoja na kunyang’anywa eneo husika na kupewa mtu mwingine.



Maelezo: MwanaHalisiOnline
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO