MwanaHalisiOnline wanaripoti...
Kutoka kushoto, Sioi Solomoni Sumari, Harry Kitillya na Shose Sinare |
Akitoa uamuzi huo Moses Mzuna, Hakimu Mfawidhi Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam amesema kuwa, rufaa hiyo haina mashiko kisheria.
“Rufaa ya shitaka hili haina miguu” amesema Hakimu Mzuna wakati akitoa uamuzi wa rufaa hiyo.
Hakimu Mzuna amesema kuwa, hoja ya upande wa utetezi ya kueleza kuwa, Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza rufaa hiyo kutokana kesi hiyo bado haijafika mwisho na kwamba, Mahakama ya Kisutu iliweza kusikiliza kesi hiyo.
Hakimu Mzuna amefuta rufaa hiyo na kwamba, kesi hiyo itaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Hakimu Mzuna amemshauri Timon Vitalis, Wakili Mkuu wa Serikali kuendelea na kesi hiyo na kwamba, endapo kesi itafika mwisho wakiwa hawajridhika na uamuzi, wanaruhusiwa kukataa rufaa.
Hata hivyo Mzuna amesema kuwa, upende wa mashitaka wanayo mamlaka ya kubadili hati ya mashtaka
CHANZO: MwanaHalisiONLINE
0 maoni:
Post a Comment