Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MEI MOSI: RAIS DKT MAGUFULI ASHUSHA KODI YA MSHAHARA KWA ASILIMIA MBILI

Moja ya mabango yaliyotumika kweye maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu
MwanaHalisiOline wanaripoti
DK. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amepunguza asilimia mbili ya kodi ya kodi ya mapato kwa wafanyakazi kutoka 11% kufikia 9%.
Magufuli ametoa agizo hilo leo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
Akitoa hotuba yake katika maadhimisho hayo, amesema Serikali yake imeamua kufikia uamuzi huo ili kuwapunguzia mzigo wafanyakazi kwani ndio kundi ambalo hawawezi kukwepa kulipa kodi.
“Watu ambao hawawezi kukwepa kulipa kodi ni wafanyakazi, ndiyo maana Serikali imeamua kupunguza mzigo huu,
“Haiwezekani mtu mwengine apate mshahara Sh. 30 milioni na mwengine apate 3,000,000 wakati anayepokea pesa ndogo ndiye anayefanyakazi kubwa, sina wivu na wanaopata mishahara mikubwa lakini nataka tunapopanda tupande wote,” amesema.
Amesema pamoja na uamuzi huo wa Serikali kupunguza makato ya kodi, ameahidi kuwa inampango wa kuongeza mishahara ili kuendelea kuwaletea nafuu wafanyakazi wanaojituma.
Amewataka wafanyakazi kupuuza wanaosema kuwa Serikali ya awamu ya tano haiwajali wafanyakazi kwani wanaosema hivyo wengi wao ndiyo wabadhilifu wanaoirudisha nyuma nchi.
“Serikali ya awamu ya tano haitambagua mfanyakazi wa aina yoyote anayefanyakazi kwa weledi,” amesema.
Hata hivyo Rais Magufuli amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa kuweka mfumo wa mishahara kuzingatia vigezo vya uzito wa kazi kwa misingi ya haki na usawa.
Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO