Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kilichosababisha Naibu Spika Kumtoa nje ya Ukumbi wa Bunge Mbunge wa Ukonga (CHADEMA), Mwita Waitara

Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson jana  aliwaamuru askari wa Bunge kumtoa Bungeni Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara baada ya mbunge huyo kutaka kumfanyia fujo mbunge wa Kasulu Vijijini Augustine Vuma Holle wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria

Jana hiyo Bungeni, Wizara ya Katiba na Sheria ilikuwa ikiwasilisha mpango wa makadirio ya bajeti kwa mwaka 2016/2017 kupitia kwa Waziri wake Harrison Mwakyembe.

Baada ya kuwasilisha kazi ikawa ni zamu ya Wabunge kuchangia bajeti hiyo, lakini hali ikabadilika wakati Mbunge wa Kasulu Vijijini Augustino Hole alivyopata nafasi ya kuchangia akaanza kwa kutoa kauli kuwa ‘Tundu Lissu ana cheti za Milembe‘ kauli ambayo ilionyesha kutowapendeza baadhi ya Wabunge wa kambi ya upinzani.

Ghafla Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara akainuka na kuanza kupiga kelele kuonyesha kutofurahishwa na kauli hiyo kisha kuanza kusimama na kuanza kupiga meza. Naibu Spika Tulia Ackson Mwansasu akamtaka mbunge huyo kukaa chini, Waitara hakuonyesha kutii amri ndipo Naibu Spika akaamulu askari Polisi wa bunge kumtoa nje ya bunge.

CHANZO: CHADEMA BLOG
Washirikishe Google Plus

About Unknown

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO