Mgogorouliosababishwa kufungwa kwa barabara ya Sokomjinga - Ngusero na wananchi wenye hasira umepata ufumbuzi baada ya madiwani wa Kata Mbili zinazotumia barabara hiyo, Mh Ally Bananga wa Kata ya Sombetini na Elirehema Nko wa Osunyai wakiwa na Mstahiki Meya wa Jiji Kalisti Lazaro na maafisa wa ujenzi Jiji kufika eneo la tukio kusikiliza wananchi hao na kuahidi kuweka bumps na alama za barabarani kupunguza janga la ajali lililokatisha maisha ya watu wa eneo hilo kwa kugongwa na magari.
Katika msafara huo wa viongozi, Katibu Tawala Wilaya ya Arusha Mjini alimwakilisha DC Nkurlu. Wengine ni maafisa wa polisi na wenyeviti wa serikali za mitaa ya Simanjiro na Banda Mbili walishiriki.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mstahiki Meya wa Jiji, matengenezo hayo yatachukua siku tano kukamilika.

0 maoni:
Post a Comment