Mbunge wa EALA, Shy-Rose Bhanji akichangia mada ndani ya bunge hilo |
Imeandikwa Na Woinde Shizza, Arusha
Serikali imekuwa inapoteza kodi nyingi zinazotokana na ushuru wa mazoao kutokana na kuwa na mzabuni mmoja ambaye anakusanya kodi za mazao kwa nchi nzima .
Hayo yamebainishwa na mbunge wa EALA, Shy-Rose Bhanji wakati akiongea na waandishi wa habari ndani ya viwanja vya bunge hilo ambapo alisema kuwa kuna changamoto kubwa ya utekelezaji wa umoja wa forodha hapa nchini Tanzania.
Alisema kuwa wafanyabiashara wengi pamoja na wakulima ambao wanazalisha mazao pamoja na bidhaa mbalimbali zinazofikia kiwango staili cha asilimia 50 %hadi 100% wanakuwa awatozwi kodi wakati wanapeleka bidhaa zao katika nchi za jumuiya wanachama.
Aidha alibainisha kuwa kuna tatizo kubwa kwa upande wa Tanzania kwani hati ambazo zinatolewa kwa ajili ya kukusanya kodi au kubaini viwango vya kusamehewa kodi zinatolewa na taaasisi moja tu ambayo ni ya tccia.
Alisema kuwa hili ni tatizo ambalo linatakiwa kutazamwa upya katika nchi yetu na serekali kwasababu TCCIA aipatikani nchi nzima bali inapatikana katika baadhi ya sehemu ambayo ni mikoa tu huku katika ngazi za wilaya pamoja na vijiji awapatikani.
Alisema kuwa hii inapelekea kodi nyingi ya mazao kupotea na pia wananchi wengi pamoja na wafanya biashara wengi kutokujua dhamana ya kodi ambayo inaweza kumuwezesha mfanyabiashara kujua unafuu wa wa kodi.
“sasa ivi ili kuweza kuwapa nafasi wananchi wengi pamoja na wafanyabishara wengi ili waweze kuelewa dhana ya unafuu wa kodi ,ni jukumu la serekali kutoa jukumu la kutoa hati hizi kwa wadau wengine ili kuleta unafuu wakodi “alisema Bhanji
Aidha alisema kuwa ili kurahisisha mambo ni vizuri ofisi za biashara za manispaa pamoja na ofisi za biashara za wialaya nawao waweze kupewa ili jukumu na wao waweze kutoa hati ambazo zitawapa nafasi wafanya biashara ambao wanasifa zinazokithi maitaji na wenye sifa kuweza kupata hati hizo .
0 maoni:
Post a Comment