Jumla ya watu 11 wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za kumbaka msishana mwenye miaka 21, kumrekodi na kusambaza picha hizo za video mtandaoni wanatarajiwa kufikishwa Mahakaman hii leo kujibu mashtaka yanayowakabili.
Kwa mujibu wa Nipashe, Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Ulirch Matei alieleza jana kuwa watuhumiwa hao wanafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Kamanda huyo amewataka wananchi kutambua kuwa sheria ya matumizi yw mitandao ipo na inafanyakazi na hivyo kuacha kusambaza picha chafu wanazopokea kupitia simu za mkononi.
Kamanda Matei alisema watuhumiwa wawili walimbaka na na kumrekodi picha za video msichana huyo bila ridhaa yake Aprili 28 mwaka huu 1 usiku katika nyumba ya kulala wageni ya Titii iliyopo eneo la Dakawa wilayani Mvomero na kisha wakazisambaza picha hizo kwenye mitandao ya kijamii ambapo watuhumiwa wengine 9 wao walishiriki kuzipokea na kuzisambaza pia.
Akifafanua zaidi alisema msichana huyo alipigiwa simu na mmoja wa watuhumiwa hao Zuber Thabit, anayedaiwa kuwa na uhusiano nae akimtaka aende katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kwamba mdada huyo alipoingia chumbani alimkuta thabiti ameshika kisu na kumuamuru kufanya kila atakachoambiwa huku akimsisitiza kutopiga kelele wala kutoa siri vinginevyo angeuawa.
Mtuhumiwa mwingine aliyeshiriki ukatili huo ni Iddy Adam (30) ambaye ndiye aliyefanyakazi ya kurekodi video hiyo.
Watuhumiwa wengine ni pamoja Rajab Salehe (26) mkazi wa Dakawa ambaye alikuwa mtu wa kwanza kutumiwa picha hizo na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Wengine waliokamatwa kwa kusambaza video hiyo ya udhalilidhaji ni Said Athumani (26), Musini Ngai (36), Said Mohammed (24), John Peter (24), Hassan Ramadhan (27), Ramadhani Ally (26), Lulu Peter (38) na Magreth Njonjome (30) wote wakazi wa tarafa ya Dakawa.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment