Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Utafiti: Vyombo vya habari vya asilia hususan magazeti vinakufa kutokana na ushindani na magazeti tando


Vyombo vya habari vya asilia hususan magazeti vinakufa. Hivi sasa vyombo hivyo vinajikongoja kutokana na  mauzo hafifu  na mdororo wa mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi. 
Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi mtandaoni  humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa Pew Research Centre unaeleza. 

Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 ("State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media), Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu. 
Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni 
 Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni change sana kuweza kutishia amani ya magazeti. 
Upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti. 
Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  ambayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.
"Ni kweli kwamba Tanzania ni bado sana kiteknolojia na miundombini kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uwongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji", amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.

Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO