Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

NE-YO AWAKOSHA MASHABIKI WA MWANZA KATIKA JEMBEKA FESTIVAL 2016


Katika kusherekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa redio ya Jembe FM iliyo na makazi yake jijini Mwanza, Mei, 21 kumefanyika tamasha lililopewa jina la JembekaFestival ambalo lilikutanisha mashabiki wa redio hiyo walio mikoa ya kanda ya ziwa kwa kupata burudani ya aina yake kutoka kwa msanii wa muziki wa miondoko ya R& B kutoka nchini Marekani, Shaffer Chimere Smith almaarufu kama NE-YO

Licha ya msanii NE-YO pia kulikuwapo na wasanii wa nchini wakiongozwa na Diamond Platinumz ambaye aliambatana na timu yake kutoka lebo yake ya Wasafi (WCB), wasanii wengine ni Fid Q, Baraka Da Prince, Ney wa Mitego, Maua Sama, Mo Music, Stamina, Juma Nature a.k.a Kiroboto, Ruby na wengine wengi.

Tamasha hilo lilifanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo pia lilihudhuriwa na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye na Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba pamoja na Mwanamitindo wa Kimataifa nchini, Flaviana Matata ambao kwa pamoja walionekana kufurahia tamasha hilo la kihistoria kuwahi kufanyika jijini Mwanza.

Kufanyika kwa tamasha hilo kulisimamiwa na mikono ya Vodacom Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu, Coca Cola, FastJet, SYSCORP, EF Outdoor, Ndege Insurance Brokers, Jembe FM, Double Tree, KK Security na Mo Entertainment ambao ndiyo waliowezesha kufanyika kwa tamasha hilo.

Kama ulikosa kuja Mwanza hii hapa video ya msanii wa muziki wa R&B kutoka nchini Marekani, NE-YO akiimba wimbo wake uliotamba na uanendelea kubamba wa 'Miss Independent".

Video ya Mkali wa Hip Hop nchini Fareed Kubanda a.k.a Fid Q akichana mistari tamasha la Jembeka na Vodacom jijijni Mwanza.

Video ya mkali wa Ragga na Dance hall, Cool Chata wa JEMBE FM ya Mwanza akiwasha moto Jembeka Festival 2016

Video msanii wa Bongo Flava, Ruby akiimba wimbo wa 'Nivumilie' kwenye tamasha la Jembeka Festival 2016.

Sebastian Ndege

Mkurugenzi mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akizungumza jambo kabla ya kuwatambulisha wageni waheshima walioshiriki kwenye Jembeka Festival 2016.(Picha zote na Modewjiblog)

RC Mwanza, John Mongella

Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba, Mbunge wa jimbo la Nyamagama jijini Mwanza, Stanislaus Mabula pamoja na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye wakimsikiliza Dr. Sebastian Ndege (hayupo pichani).

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanislaus Mabula

Mbunge wa jimbo la Nyamagama jijini Mwanza, Stanislaus Mabula akizungumza machache katika Jembeka Festival 2016 kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye kuwasalimia wakazi wa jiji Mwanza waliofurika katik uwanja wa CCM Kirumba mwishoni mwa wiki.

Nape Nnauye

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) na kubariki tamasha la Jembeka Festival 2016 lililofanyika katika viwanja vya CCM Kirumba jijini humo.

Costantine Magavilla

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Jembeka Festival 2016, Costantine Magavilla akisamiana na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye.

Dr. Sebastian Ndege

Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege akibadilishana mawazo na mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye pamoja na Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba wakati burudani zikiendelea kwenye Jembeka Festival 2016.

Mh. Nape Nnauye

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye (katikati) akifafanua jambo kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Jembe Media Group, Dr. Sebastian Ndege (kulia) pamoja Waziri Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba.

Jackson StarTimes

Wadau wakifuatilia burudani mbalimbali zilizokuwa zikiendelea.

Jembeka Festival 2016

Vijana wa Mwanza walikuwepo kumshuhudia msanii Neyo Live kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Monica Joseph

Mbunge wa jimbo la Nyamagama jijini Mwanza, Stanislaus Mabula (kushoto) na Mtaalamu wa masuala ya fedha nchini, Monica Joseph (wa pili kushoto) walikuwepo kushuhudia tamasha la Jembeka na Vodacom ililoweka historia jijini Mwanza 2016. Kwa picha zaidi bofya hapa

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO