Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari amelazimika kukosa ushiriki wa vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma na badala yake kulazimika kurudi Jimboni kwake ili kusaidia kufariji wanafunzi, walimu na wazazi kufuatia kuungua moto kwa bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari Kikatiti.
Katika ajali hiyo ya moto hakuna mwanafunzi aliyeuumia au kupoteza maisha. Blogu hii haijaweza kupata thamani halisi ya hasara ya moto huo. Tunaendelea kufuatilia na tutakujuza hapahapa.
Katiba bandiko lake kwenye mtandao wa Facebook Mh Nassari ameandika haya
"Natoa pole nyingi kwa Shule ya Kikatiti Sec. kwa janga la kuungua bweni la wavulana.
Nimelazimika kuacha bunge kuja kuwaona. Tunamshukuru sana Mungu kwakuwa hakuna mwanafunzi aliyejuruhiwa wala kupoteza maisha. Together we stand, together we go"
Mh Joshua Nassari akifurahia jambo na baadhi ya wanafunzi wa Sekondari ya Kikatiti |
Mh Nassari akizungumza na walimu na wanafunzi wa Sekondari ya Kikatiti alipoenda kutoa msaada na kufariji wahanga |
Sehemu ya bweni la wavulana liliotekekezwa kwa moto. Pichani baadhi ya mafundi wakiendelea na ukarabati wa paa ambalo lilimalizika kabisa |
Mh Nassari akiangalia uharibifu wa moto kwenye bweni la wavulana Sekeondari ya Kikatiti |
Mh Nassari akifurahi pamoja na wanafunzi wa Sekondari ya Kikatiti baada ya kuwakabidhi misaada ya kibinadamu yakiwemo magodoro na shuka kufuatia bweni la wavulana kuungua na moto |
0 maoni:
Post a Comment