Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimkaribisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika Mei 27, Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere.
Mhe. Waziri Mahiga akiwahutubia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara. Katika hotuba yake aliwaasa watumishi kuwa waadilifu, kufanyanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuhakikisha shughuli za kidiplomasia zinafanyika kwa tija ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Sera ya Mambo ya Nje inatekelezwa na kuifanya Tanzania kuendelea kupaa katika medani za kimataifa.
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akitoa taarifa ya utangulizi ya mkutano kwa Mhe. Waziri, Viongozi wa TUGHE-Taifa pamoja na wafanyakazi waliohudhuria Mkutano huo hawapo pichani. Pia alitumia fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Waziri ili aweze kufanya ufunguzi wa Mkutano ambapo tukio hilo liliambatana na utoaji wa zawadi za wafanyakazi bora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Sehemu ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Kilima akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mahiga kwa niaba ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pamoja na kuahidi kufanyia kazi nasaha zilizotolewa, Balozi Kilima alimpongeza Waziri Mahiga kwa kuwa kiongozi bora na wa mfano wa kuigwa na Watumishi wote katika utendaji wa kazi.
Mjumbe kutoka TUGHE-Taifa, Bw. Arcado Nchinga pia alizungumza na Watumishi wa Wizara ambapo aliwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaiwakilisha nchi vizuri katika mataifa mengine.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Bw. Nigel Msangi akitoa taarifa ya wafanyakazi bora wa Wizara wa mwaka 2015/2016 kwa Waziri Mahiga ambao walitunukiwa zawadi katika mkutano huo.
Afisa Habari katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Ally Kondo ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pichani akipongezwa na Mhe. Waziri Mahiga.
Afisa TEHAMA katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw.Salum M. Nalolah ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pichani akipongezwa na Mhe. Waziri Mahiga.
Picha ya pamoja ya Mhe. Waziri na Wafanyakazi bora wa Idara zote za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Picha ya pamoja Mhe. Waziri Mahiga na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
PICHA NA STORI: ISSA MICHUZI
PICHA NA STORI: ISSA MICHUZI
0 maoni:
Post a Comment