Kampuni ya StarTimes tawi la Arusha imefungua ofisi mpya ya huduma kwa wateja eneo la Florida katika Kata ya Levolosi ya Jiji la Arusha, ofisi ambayo imeziduliwa rasmi na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Mh Kalisti Lazaro leo.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Meya wa Jiji la Arusha, Mh Kalisti aliwashukuru Startimes kwa kumpa heshima ya kuzindua ofisi yao na kuwaomba waendele kutoa huduma bora kwa wateja.
Mh Kalisti aliwaasa vijana waliobahatika kupata ajira katika Kampuni ya StarTimes kufanya kazi kwa bidii na uaminifu katika kuwahudumia watanzania na kwamba ofisi yake huru kutoa ushirikiano utakaohitajika muda wowote. Aidha, alieleza kuwa Halmashauri anayoiongoza itajitahidi kuendelea kuweka mazingira maazuri ya uwekezaji ili kutoa fursa za ajira kwa vijana.
Katika uzinduzi huo, Meneja wa Startimes Kanda ya Kaskazini inayounganisha mikoa ya Arusha, Bw Kelvin alimshukuru Meya huyo wa Jiji kwa kukubali mwaliko wa StarTimes na kushiriki ufunguzi wa ofisi katika siku isiyo ya kazi kiofisi, kueleza kwamba lengo la kufungua ofisi hiyo mpya ni kufikisha huduma karibu zaidi na wananchi katika muda mfupi na kwa gharama nafuu.
Meneja huyo wa Kanda alimhakikishia Mstahiki Meya wa Jiji na wananchi wa Arusha kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wa StarTimes lengo likiwa ni kuhakikisha kila mkazi wa Jiji la Arusha anaweza kuipata huduma ya StarTimes kwe bei anayoimudu na kwa ubora mkubwa zaidi.
Akifafanua zaidi, Bw Kelvin alisema kwasasa kampuni yake ya StarTimes inauza ving'amuzi vya kawaida kwa bei nafu ya shilingi 22,000/= na vile vya dishi wanaviuza kwa shilingi 86,000/= vyote vikiambatana za nyongeza ya muda wa matumizi uliolipiwa na bila gharama za ufundi.
Akifafanua zaidi, Bw Kelvin alisema kwasasa kampuni yake ya StarTimes inauza ving'amuzi vya kawaida kwa bei nafu ya shilingi 22,000/= na vile vya dishi wanaviuza kwa shilingi 86,000/= vyote vikiambatana za nyongeza ya muda wa matumizi uliolipiwa na bila gharama za ufundi.
0 maoni:
Post a Comment