Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA ZAIDI: ZIARA YA KATIBU MKUU WA CHADEMA DK MASHINJI NA UJUMBE WAKE WALIPOTEMBELEA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Vincent Mashinji (katikati) akizungumza na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh Daniel Kidega (kulia) ofisini kwake alipotembelea ofisi hizo zilizoko Jijini Arusha jana. Kulia kwake ni mjumbe wa kamati Kuu ya chama hicho ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Mh Fredrick Sumaye.
Picha na Grace Macha, the Professional Jounalist

Msafara wa viongozi walioambatana na Dk Mashinji ukilakiwa na mwenyejei wao Spika wa EALA Mh Kidega (mwenye suti ya khaki na tai mbele). Wegine mstari wa mbele, kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa, Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Profes Baregu, anafuatia Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha ambaye pia ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Mh Kalisti Lazaro Bukhay aliye kushoto kwa spika. Picha na Grace Macha, the Professional Jounalist


Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Vincent Mashinji (kulia) akisalimiana na Mbunge mwakilishi wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki Mh Charles Makongoro Nyerere 


Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akizungumza katika ikao cha pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki katika sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Mashinji kutembelea ofisi hizo jana. Picha na Grace Macha, the Professional Jounalist
Spika wa Bunge la jumuia ya Afrika Mashariki Mh Daniel Kidega akizungumza na wageni wake jana
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mh Makongoro Nyerere akielekeza jambo kwa waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA katika ziara ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa CHADEMA kwenye ofisi hizo Jijini Arusha jana. 
Picha na Grace Macha, the Professional Jounalist


Washirikishe Google Plus

About SeriaJr TW

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO