Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

MWENYEKITI WA CCM, RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AKAGUA DARAJA LA NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM, LEO


 Mweneyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipewa maelezo ya awali na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alipowasili kukagua daraja lla Nyerere, leo Mei 10, 2016. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga, akimpokea Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipowasili kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza na viongozi mbalimbali waliompokea, kabla ya kukagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara zinazopishana ya chini na ya juu mwanzoni mwa daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo, leo
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama barabara zinazopishana ya chini na ya juu mwanzoni mwa daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo, leo
 Msafara wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ukipita kwenye daraja la Nyerere kwenda Kigamboni, alipokagua daraja hilo leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu jakaya Kikwete akiangaza mandhari ya darala la Nyerere alipokagua daraja hilo leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimuuliza jambo,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga (kulia), wakati akikagua daraja la Nyerere leo Kulia kwake ni Mama Salma Kikwete 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu kwenye daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama salma Kikwete wakitembea kwenye daraja hilo leo. ushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipita eneo ambalo magari yatakuwa yakilipia ushuri, alipokagua daraja la Nyerere, leo 
 Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitazama moja ya  ofisi zitakazotumiwa na magari kulipia ushuru wa kutumia daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo Mei 10, 2016
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsalimia Ofisa Uhusiano wa NSSF, Kiamba Rajabu, alipokagua daraja la Nyerere, Dar es Salaam, leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Mipango na Ujenzi wa NSSF, Yakub Kidula,  kuhusu eneo la magari kulipia ushuru alipokuwa akikagua daraja la Nyerere leo. Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na akipatiwa maelezo na Mkurugenzi wa Mipango na Ujenzi wa NSSF, Yakub Kidula,  kuhusu eneo la magari kulipia ushuru alipokuwa akikagua daraja la Nyerere leo. Kulia ni Mama Salma Kikwete
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipanda ngazi kwenda kwenye ofisi za Utawala unaosimamia utoaji huduma za daraja la Nyerere, alipokagua daraja hilo leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama salma Kikwete wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na uongozi unaosimamia huduma za daraja la Nyerere baada ya kukagua daraja hilo leo
 Dajala hilo la Nyerere na barabara zake linavyoonekama
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Mama salma Kikwete wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na uongozi unaosimamia huduma za daraja la Nyerere baada ya kukagua daraja hilo leo. Kushoto kwa Jkk ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga








Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitoa maneno ya shukurani kabla ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu jakaya Kikwete kuondoka baada ya kukagua Daraja la Nyerere leo. Daraja hilo ambalo lilianza kujengwa wakati Kikwete anamalizia awamu ya mwisho ya uongozi wake wa Urais, limefunguliwa hivi karibuni na Rais wa awamu ya tano Dk. John Magufuli baada ya kukamilika. 
STORI&PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, leo amekagua Daraja la Nyerere, Kigamboni, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kuona mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya CCM. 

Baada ya kuwasili kwenye daraja hilo, Dk. Kikwete akifuatana na Mkewe Mama Salma, alipokewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Joseph Nyamhanga, na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambapo mwanzoni alikagua miundombinu na kisha kutembea kwa miguu kwenye daraja hilo, huku Katibu Mkuu huyo akimpatia maelezo mbalimbali kuhusu daraja hilo.

Nyamhanga alimwabia Dk. Kikwete kwamba  Mei 14, mwaka huu, serikali itaanza kutoza tozo kwa vyombo vya usafiri vitakavyopita katika daraja hilo la Nyerere kwa lengo la kufidia gharama za matunzo na usimamizi wa endeshaji wa huduma za daraja hilo.

“ Baada ya kufunguliwa kwa daraja hili na kuanza kutumika kwa kupita bila kulipa kwa vyombo vya usafiri  tangu Aprili 19  2016 na sasa tunaanza rasmi kutoza tozo kwa ajili ya kukusanya gharama za usimamizi, utunzaji na uendeshaji wa daraja hili.” alisema Nyamhanga.

Nyamhanga alimwambia Dk. Kikwete kwamba watembea kwa miguu watapita bure katika daraja hilo huku wenye baiskeli wakilipia Sh. 300, pikipiki Sh. 600, waendesha maguta, bajaji na magari ya kawaida (Saloon Cars) watatakiwa kulipia Sh.1500.Mabasi yanayobeba  abiria 15 yatalipia  Sh. 3,000, yale ya abiria zaidi ya 15  Sh. 5,000  na yale yanayobeba  abiria zaidi  ya 29 yatalipia Sh. 7,000.

Aidha magari yenye tani zaidi ya mbili mpaka saba yatalipia Sh. 7,000, tani 7 hadi 15 watalipa Sh.10,000, tani 15 mpaka 20 watalipa Sh.15,000  na yale yenye  tani 20 mpaka 30 yatalipia Sh. 20,000.

Nyamhanga aliongeza kwamba kuwa magari yenye namba za Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Polisi (PT), Jeshi la Magereza (MT), magari yakubeba wagonjwa, magari ya zimamoto na magari yenye vibali maalum yataruhusiwa kupita bure.

Daraja hilo la Nyerere, ambalo awali lilifahamika kwa jina la Daraja la Kigamboni, limejengwa wakati Dk. Kikwete akiwa katika awamu ya mwisho ya uongozi wake wa Urais, na lilizinduliwa hivi karibuni na Rais Dk. John Magufuli na kulipa daraja hilo jina la Nyerere.
Washirikishe Google Plus

About Ujenzi Connekt

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO