Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kesi dhidi ya Lema (Mb) ya uchochezi Chuoni yaahirishwa hadi Oktoba 1, 2013; OCD, Makamu Mkuu wa Chuo Mashahidi Muhimu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha shauri la kesi inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mh Godbless Lema (CHADEMA), kwa tuhuma za kuchochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)  hadi Octoba 1, 2013 ambapo mashahidi wa upande wa mashitaka wataanza kutoa ushahidi wao kwa siku mbili mfululizo.

Akitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi Hakimu Mkazi Hawa Mguruta alisema kwamba ameridhia ombi la Wakili wa Mh Lema aliyeomba shauri hilo liahirishwe kutokana na mteja wake kuwa mgonjwa. Hakimu Msofe aliwataka mashahidi wote kama walivyohuduria leo kufika Mahakamani hapo siku ya Jumanne na Jumatano ya Oktoba 1 na 2 kwa ajili ya kuanza kutoa ushahidi wao, zoezi ambalo lilipangwa kuanza leo kama kuningekuwa na udhuru wa kuahirisha shauri hilo.

Mashahidi wa upande wa Jamhuri waliofika Mahakamani hapo ni pamoja na OCD wa Wilaya ya Arusha Mjini, Giresi Muroto na Mlezi wa Wananfunzi chuoni hapo Bw John Joseph Nanyaro.

Wengine ni maofisa wa Polisi Bernad Nyambalya na Jane Chibuga; na Makamu Mkuu wa Chuo cha IAA Bw Faraj Kasidi.

Awali Wakili Kimomongoro anayemwakilisha Lema wakisaidiana na Wakili Humrefy Mtui aliwasilisha ombi la kuiomba Mahakama iahirishe shauri hilo hadi tarehe nyingine kwa kile alichoeleza kuwa ni kutokana na Mh Lema kuwa katika hali ya kuumwa na kwamba ni jana tu aliruhusiwa kutoka hospitali ya AICC alikokuwa amelazwa tangia Agosti 14 akiendelea kutumikia siku 10 alizopewa na daktari za mapumziko ya kitandani.

Wakili Kimomongoro alimkabidhi mwanasheria wa Jamhuri nakala ya “Discharge Summary” kutoka hospitali ya AICC nae akaipitia na kuridhia shauri hilo kuahirishwa kutokana na sababu hiyo ya ugonjwa.

DSC09072Mashahidi wa kesi hiyo ya uchochezi dhidi ya Lema wakiondoka katika viwanja vya Mahakama leo hii asubuhi. Kwa nyuma anaonekana Dean of Students akizungumza na Inspekta Bernad.

DSC09071Mashahidi upande wa mashitaka. anaeongea na simu ni Makamu Mkuu wa Chuo cha IAA, Bw Faraj Kasidi na anaemtazama ni Jane Chibuga.

DSC09074OCD Giresi Muroto akisalimiana na dereva wa gari ya Mbunge Lema huku Wakili Mtui akishuhudia nje ya viwanja vya Mahakama Kuu Arusha.

DSC09076Inspekta Bernad Nyambalya akisalimiana na Mawakili wa Mh Lema mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa. Kulia kabisa ni Mwanasheria Glory Kaaya. Picha zote na Seria Jr.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO