Miaka ya karibuni, matukio ya watu mbalimbali kumwagiwa tindikali inayoweza kuwasababishia ulemavu ama kifo yameongezeka kwa kasi kiasi cha kuonekana kama ni jambo la kawaida tu.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania, Dk. Eliezer Feleshi na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samweli Manyele walitoa tamko la kudhibiti upatikanaji holela wa tindikali ambao umesababisha kujeruhiwa kwa watu wengi nchini.
Blog hii inatoa rai kwa raia wote wa nchi hii kuwa wamoja na kusaidiana na vyombo vya usalama katika kuhakikisha ukatili huu haupati nafasi tena katika jamii yetu.
Mmiliki wa Home Shopping Centre akiwa na majeraha ya kumwagiwa kemikali hiyo
Kijana huyu alimwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa Igunga, baadae tukio lake likachukuliwa kisiasa zaidi na kushindwa kufahamika walengwa hasa ni kina nani
Global Publishers walipata kuripoti kuwa kuna baadhi ya walimu wa maabara wanauza bidhaa hiyo mtaani
Mitaani watu wanasema tindikali ni silaha mpya ya maangamizi kwa kizazi cha sasa ambapo kila kukicha hofu ya watu kujeruhiwa na kimiminika hicho inazidi kupanda.
Mpaka sasa, Watanzania wengi wameshamwagiwa tindikali na watu wanaosadikiwa ni wabaya wao. Miongoni mwa watu waliokumbwa na balaa hilo ni mmiliki wa Home Shopping Center, Said Mohamed Saad, Shehe wa Bakwata wilayani Arumeru, Issa Makamba na mtu aliyedaiwa ni mpiga debe wa CCM, Igunga Mussa Tesha.
Wengine ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Katibu wa Mufti Zanzibar, Shehe Fadhili Soraga na wasichana wawili raia wa Uingereza, Kirstie Trup na Katie Gee.
Picha: Makusanyo toka vyanzo mbalimbali
0 maoni:
Post a Comment