Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Kamati ya Kulinda Waandishi Afrika yatoa Ripoti inayoikosoa Tanzania kuhusu Uhuru wa Vyombo vya Habari

 

Nairobi.

Serikali ya Tanzania imekosolewa na kutiliwa shaka kuhusu uwazi na demokrasia kutokana na kubana uhuru wa habari na kuvifuatilia baadhi ya vyombo vya habari.

Hiyo imo katika ripoti iliyowasilishwa na Kamati ya Kulinda Waandishi (Committee to Protect Journalists) kwa nchi za Afrika, ambayo imeeleza kwamba Tanzania haina uhuru wa habari kama inavyoelezwa kutokana na kufuatiliwa kwa waandishi mmoja mmoja, hivyo kuingilia uhuru wa watu kupata habari.

“Kuongezeka kwa matukio ya kushambuliwa kwa waandishi wa habari hivi karibuni na kuwapo kwa sheria zinazobana uhuru wa habari, kunawafanya waandishi wa habari kuzidi kuhofia usalama wao wawapo kazini. Na suala la kuwafuatilia mmojammoja inamaanisha kuzuia taarifa kuwafikia wananchi,” alieleza Tom Rhodes, mtaalamu wa ushauri wa CPJ kwa nchi za Afrika Mashariki.

Serikali imekuwa katika mchakato wa kutaka kurekebisha sheria zinazosimamia uhuru wa habari na tayari imeshatia saini makubaliano ya ushirikiano wa wazi baina ya Serikali na wadau wa habari, kwa ajili ya kuongeza juhudi za kuimarisha uwazi.

Ripoti hiyo imeainisha kwamba uhuru huo unaingia kwenye dosari kutokana na mauaji ya aliyekuwa mpigapicha wa Televisheni ya Channel Ten, Daudi Mwangosi na kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi pamoja na kushambuliwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji wa New habari, Absalom Kibanda na kutishiwa kuuawa kwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi.

Source: Mwananchi

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO