Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Lema, Nassari washiriki kuaga mwili wa “Redbrigade” wa Chadema Usa River aliyefariki kwa matatizo ya tumbo

DSC08592

Baadhi ya walinzi wa amani wa Chadema Jijini Arusha kutoka kitengo cha chama maarufu kama Brigedia Nyekundu wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwenzao Privatus Lazaro Mahabusi (38) kutoka katika chumba cha kuhifadhia maiti hopsitali ya Mt Meru mapema leo asubuhi kwa ajili ya zoezi la ndugu jamaa na marafiki kuaga mwili huo. Privatus alifariki siku ya Jumamosi Agost 10, 2013 katika hopsitali ya Selian Jijini hapa alikolazwa kwa matatizo ya vidonda vya tumbo.

Kwa mujibu wa mratibu wa shughuli za maziko, mwili wa marehemu utasafirishwa hadi Mahenge Morogoro kwa maziko baada ya shughuli za misa na na kuaga mwili huo kumalizika nyumbani kwake Usa River – Ngaresero.

Blog hii iliweza kutembelea nyumbani kwa marehemu jana ambapo msiba ndipo ulipo na kubahatika kuonana na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari akiwa katika pilikapilika za kuhakikisha mambo yanakaa sawa ili kufanikisha zoezi la kuusitiri mwili wa marehemu kwenye nyumba ya milelele na pia kuweka utaratibu wa kumsaidia mjane na watoto walioachwa.

Kabla yake Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema, Katibu wa Chama Wilaya Mh Martin Sarungi, Mjumbe wa Kamati ya Chadema Kanda ya Kaskazini Mh Chris Mbajo na viongozi wengine walifika nyumbani kwa marehemu kuhani wafiwa.

Marehemu ameacha mke na watoto watatu, wawili wakiume na mmoja wa kike.

DSC08597

 

DSC08590Baadhi ya viongozi ambao hawakuweza kusafiri hadi Usa River wakitoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao katika hopsitali ya Mt Meru. Mwenye kombati nyeusi ni Diwani wa Chadema kutoka Arumeru Magharibi, Mh Gibson na kulia kwake ni Katibu wa Wilaya Martini Sarungi akifuatiwa na Mh Hilary kutoka Chadema Mkoa.

DSC08591

DSC08595Mh Lema akishuhudia jeneza lenye mwili wa marehemu likipakiwa garini tayari kwa safari

DSC08594Mbunge akiwa na sura ya huzuni kwa kuondokewa na kijana wake mpambanaji

DSC08593

DSC08602

Gari ya chama iliyobeba jeneza la mwili wa marehemu likiondoka viwanja vya Hospitali ya Mt Meru kuelekea Usa River.

Kishili na LemaMwenyekiti wa Vijana Chadema na Katibu wa Chadema Arumeru Mashariki, Bw Methew Kishili akimuelekeza jambo Mbunge Lema katika viwanja vya hopsitali ya Mt Meru wakisubiri mwili wa marehemu.

DSC08604Msafara ukiondoka hospitalini hapo kuelekea Usar River ambapo misa ya kumuaga marehemu na kutoa heshima za mwisho itafanyika kabla ya safari ya kuelekea Morogoro. Mh Lema na Mh Nassari pamoja na viongozi wengine wa Chama Mkoa na Wilaya ya Arumeru watashiriki katika ibada hiyo na zoezi la kuaga mwili wa marehemu.

Nassari, LemaMh Lema na Mh Nassari wakiwa nyumbani kwa marehemu katika zoezi la kuaga mwili kabla ya safari ya kuelekea Morogoro. Wengine waliokaa ni Bw Alphonce Mawazo na Joseph Moses kulia kabisa.

Mtoto mkubwa marehemu

Jeneza lenye mwili wa marehemu nyumban kwake

Mke wa marehemu Privatus (mwenye kilemba cheupe)

Mwenyekiti wa Chadema Arumeru Mashariki akitoa salamu za pole kwa niaba ya chama Wilaya

Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akitoa nasaha zake wakati wa kuaga mwili wa marehemu kwa ajili ya safari ya kuelekea Morogoro kwa maziko.

ENZI ZA UHAI WAKE

PrivatusHapa ni enzi za uhai wake akiwa eneo la Mahakama Kuu Jijini Arusha (mwenye t-shirt ya M4C) na watunza amani na usalama wenzake wa chama katika moja ya kesi za Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema. Marehemu ameacha mke na watoto watatu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO