Pichani ni mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chadema, Mh Godbless Lema akihutubia mamia ya wakazi wa Kata ya Baraa katika mkutano wake leo jioni kufuatlia shughuli za maendeleo Jimboni kwake, hasa ujenzi wa Kituo cha afya cha katika Kata ya Baraa.
Wakati huo huo.. Diwani Mteule Kata ya Kaloleni amefanya mkutano wa kuwashukuru wananchi waliomchagua
Kamanda wa Chadema, Ally Bananga akiwashukuru wananchi wa Kaloleni kwa kuichagua Chadema Kata ya Kololeni katika uchaguzi uliofanyika Julai 14, 2013 na Chadema kuibuka washindi kwa tofauti kubwa ya kura dhidi ya CCM na CUF na kunyakua Kata zote nne zilizokuwa zinashindaniwa (Kaloleni, Kimandolu, Themi na Elerai)
Bananga katika hotuba yake, amemhusia Diwani wa mteule wa Kaloleni Mh Emmanuel Kessy kwa kumkumbusha kwamba Chadema ni chama chenye ujasiri wa kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya cham na taifa na hivyo kama atafanya mzaha na wajibu aliokabidhiwa kuwatumikia wananchi atashughulikiwa “Chadema ni chama cha maamuzi magumu ukileta mchezo tunakaka mti tunapanda mti”, amesema Ally Bananga
0 maoni:
Post a Comment