Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa akifafanua jambo katika Kikao cha Mkutano wa Baraza la Katiba kwa upande wa Chadema kama taasisi ya kisiasa kukusanya maoni na mapendekezo juu ya Rasimu ya Katiba Mpya. Kushoto kwake ni Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini ambae pia ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Mh mani Golugwa na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Mh Samson Mwigamba.
Kikao hiki kilifanyika katika hoteli ya New Arusha na kuhudhuriwa na wananchi mbali mabli hasa waliokosa nafasi kutoa maoni yao katika mkutano wa wazi mchana katika viwanja vya Kilombero Jijini hapa. Miongoni mwa watu amshuhuri ambao walihudhuria tukio hili hapo hotelini ni pamoja na Wakili Mabere Marando, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Dk Kitila Mkumbo na Mratibu wa Ukusanyaji maoni kwa Chadema, Mh Mwikwabe Mwita Waitara.
Wengine ni wanasheria mbalimbali wa Jijini Arusha wakiongozwa na Mawakili Kimomongolo na Henry Mtui, wasomi mbali mbali, wafanya biashara, na wnataaluma wengine, bila kusahahu baadhi ya madiwani wa Chadema Mkoani Arusha.
Pichani kushoto anaonekana Mjumbe wa Baraza la Kanda ya Kasakazini, Mh Chris Mbajo
Baadhi ya wajumbe wakitoa maoni yao kwa kujaza kwenye fomu maalumu kutokana na nafasi haba za kuchangia kwa kuongea kutokana na uwingi wa watu. Msaidizi wa Mbunge wa Arusha Mjini kwatika maswala ya usafiri, Bw Haleluya aking’aa na vazi lake kama rubani wa chopa..
Utulivu na umakini katika kufuatilia zoezi la utoaji maoni
Wakili mkongwe na nguli wa Sheria ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando akifafanua maswala mbalimbali ya kisheria kuelekea katika zoezi la ukusanyaji maoni ya Rasimu ya Katiba mpya
Dr Kitila Mkumbo nae alipata wasaa wa kusema neno. Dr Kitila aligusia umuhimu wa wananchi na Serikali kwa ujumla kuhakikisha inapatikana Katiba Mpya ambayo itakuwa ni kwa maslahi ya watanzania wote. Aidha alitahadharisha uwezekano wa Chama Tawala kutofanikisha mchakato huu vizuri kutokana na alichodai kulazimishwa na umma kuingia kwenye mchakato wa Katiba mpya na dalili ziliozanza kujionesha kwa chama hicho kupingana kwa karibu asilimia 80 ya mapendekezo ya Rasimu ya Katiba mpya ambyao kwa upande wa Chadema wanayaunga mkono kwa kiwango kikubwa.
Wakili Komomongolo akitoa maoni yake na kushauri uwekwe utaratibu wa kisheria kumzuai DPP (Mwendesha Mashtaka wa Serikali) kutokuwa na nafasi ya kujiamulia tu kufuta kesi namna apendavyo. Kimomongoro alishauri Katiba itamke uwepo utaratibu wa kimahakama ambapo kama DPP atataka kufuta kesi fulani anaiandikia Mahakama na kutoa sababu husika za nia ya kufuta kesi fulani. Alisema hii itasaidia kuzuia kuwa na kesi nyingi za kutengeneza na kubambikizia wananchi ambazo mara nyingi hupoteza muda wa watu na fedha nyingi ila sababu na baadae kuishia kufutwa.
Profesa Mushi kutoka Chuo Kikuu cha teknolojia cha Nelson Mandela kilichopo Tengeru Jijini hapa akitoa mapendekezo yake na ushauri kwa Chadema. Profesa huyu alidai Chadema ndio utamaduni na maisha yake tangia kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
Mzee maarufu Jijini hapa kama “Baba Bonny” ambae alitambulishwa na Katibu wa Chadema Arusha kuwa ni mtu aliyesaidia sana Chadema kushinda Kata ya Daraja mbili mwaka jana akitoa maoni yake. Mzee huyu pamoja na mabo mengi aligusia zaidi uhuru wa wananchi kufaidi ardhi yao na mavuno yatokayo shambani na kupinga vikali utaratibu wa sasa wa ukamataji na utaifishaji wa mali zinazokamatwa mpakani.
Mwanadada Doris Cornel akichangia maoni yake ambapo alishauri katiaka sheria za uchaguzi na upigaji kura umri wa kuandikisha wapiga kura kama ni kuanzia miaka 18 basi zoezi la uandikishaji lihusihe hata walio na miaka 17 ili kuwapa muda mwaka unaofuata kushiriki uchaguzi kwa vile watakuwa na miaka 18 kamili.
Diwani mteule wa Kata ya Kaloleni, Mh Kessy nae alipata fursa ya kutoa maoni yake kwa kuongea.
Mdau wa mtandao maarufu wa kijamii maarufu kama “JamiiForums”, Bw Mungi alikuwa miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo wa ndani. Bw Mungi amekuwa akiripoti matukio mengi “live” yanayotokea Jijini hapa kupitia mtandao huo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Mkoa wa Arusha, Mh Cecilia Ndosi akitabasamu baada ya kumulikwa na kamera yetu akijaza maoni yake kwenye fomu maalumu katika mkutano huo
Hawa ni baadhi ya wanasheria vijana waliohudhuria kikao hicho. Mwenye suti nyeusi katikati ni Mwanasheria James Lyatuu na kushoto kwame ni Mwanasheria Wakili Humphrey Mtui
Bossi Mzito wa Blog hii, SeriaJr akiwa busy ndani ya ukumbi wa mkutano huo Hotel ya New Arusha akifanya yake..
0 maoni:
Post a Comment