Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Hatima makada wa Chadema Agosti 5

kilewo

Mawakili wa pande zote wametoa maelezo yao huku upande wa Henry Kilewo na wenzake ukiitaka Mahakama Kuu ifute mashtaka yanayowakabili kutokana na kutokuwa na uhalali wa kisheria.
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imepanga kuwa itatoa maamuzi yake juu ya shauri hilo ifikapo Agosti tano mwaka huu.


Uamuzi dhidi ya kesi inayowakabili wanachama watano wa Chadema yaliyokuwa yatolewe jana sasa yatatolewa Agosti 5. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Simon Lukelelwa alitoa uamuzi huo kufuatia kuchelewa kufika kwa washtakiwa wa kesi hiyo waliohifadhiwa Gereza la Uyui Tabora.

Wakati uamuzi huo ukitolewa na Jaji Lukelelwa, washtakiwa wote watano wa kesi hiyo, Henry John Kileo, Evodius Justian, Oscar Kaijage, Seif Kabuta na Rajab Kihawa hawakuwa katika chumba cha mahakama muda wa saa tatu na nusu asubuhi.

Washtakiwa walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa nne na dakika arobaini na waliarifiwa na wakili mwakilishi, Emanuel Msyani kuwa shauri limepangwa tarehe tano mwezi ujao wakiwa ndani ya chumba cha mahabusu ya Mahakama Kuu.

Wakili Msyami alisema Mahakama Kuu iliridhia ombi la upande wa Jamhuri kuomba kuongezewa muda angalau kwa siku moja kwa vile walipokea hoja Ijumaa iliyopita.

Aliongeza kuwa Mahakama Kuu ilikubali ombi hilo na kuongeza muda hadi tarehe moja uwe umewasilisha majibu ya hoja na kuipanga tarehe tano kwa ajili ya uamuzi.

Kesi hiyo ya rufaa ya jinai namba 53/2012 ilifunguliwa na Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala na kuanza kusikilizwa Julai 22 mwaka huu mbele ya Jaji Lukelelwa ikiomba miongozo ya kisheria ikiwemo yaliyotolewa na mahakama za wilaya na mkoa.

Shauri la maombi ya marejeo liliwakilishwa na Wakili Peter Kibatala anayewatetea washitakiwa, akiiomba mahakama kuu ipitie majalada ya kesi mbili dhidi ya wateja wake zilizofunguliwa mahakama hizo baada ya kuona maamuzi yake hayakutenda haki.

Wakili Kibatala alibainisha katika maombi hayo kwamba kutokana na maamuzi hayo ya mahakama za chini yameathiri pia haki za waomba rufaa ikiwa ni pamoja na kuwanyima haki ya kupata dhamana.

Kwa upande wake Serikali ilishindwa kujibu maombi hayo, badala yake ilijenga hoja kwamba walichelewa kupata nyaraka hizo kwani walizipokea siku moja kabla ya kutajwa shauri hilo hivyo walishinda kuzijibu.

Chanzo: Chadema Blog

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO