Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

TASWIRA: MKUTANO WA BARAZA LA KITAASISI LA CHADEMA KWA MAONI YA RASIMU YA KATIBA LILILOONGOZWA NA DR SLAA JIJINI ARUSHA LEO

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr Wilbroad Slaa akizungumza na wananchi wa Jijini Arusha jioni ya leo katika muendelezo wa Mikutano ya wazi ya Mabaraza ya Kitaasisi ya Chadema kukusanya maoni ya Katiba Mpya kwa upande wa Chadema kama taasisi kamili.

Dr Slaa kwa siku ya leo amefanikiwa kufanya mikutano miine ya wazi Mkoani Arusha na baadae kushiriki katika kikao kingine cha mabaraza hayo cha ndani kilinachoendelea katika hoteli ya New Arusha.

Katika mikutano hiyo Dr Slaa ameambatana na wanasheria wa chama akiwemo Mabere Marando pamoja na viongozi wengine kutoka makao makuu akiwemo mjumbe wa Kamati Kuu Dr Kitila Mkumbo.

Wananchi mbali mbali walipata fursa ya kutoa maoni yao hadharani katika mjumuiko huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi, na kujaza eneo la wazi katika viwanja vya Kilombero Jijini hapa.

Chadema wamepanga kuzunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ya Tanzania wakiwa na lengo la kukusanya maoni ya watu wasiopungua milioni 8. Tayari viongozi mbalimbali wa chama hicho wametawanyika maeneo tofauti ya nchi kuendesha vikao vya mabaraza hayo.

Awali wanasheria mbalimbali wa chama Mkoa wa Arusha walikuwa wakiwaelimisha wananchi masuala mbali mbali kuhusiana na Katiba na sheria kwa ujumla katika kuwaanda vyema kabla ya kutoa maoni yao.

Dr Slaa akiwasili katika viwanja vya Kilombero Jijini Arusha

Mratibu wa vikao vya mabaraza ya Chadema, mh Mwita Waitara akisalimia wananchi kabla ya kumkaribisha Wakili Mabere Marando ambye pia alimkaribisha Dk Slaa

Mwanasheria wa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama, Wakili Mabere Marando akichambua baadhi ya vifungu vya rasimu ya Katiba inayokusudiwa kutolewa maoni na wananchi. Marando amesema kwa upande wa Chadema wanaunga mkono zaidi ya asilimia 80 ya mambo yaliyomo katika rasimu hiyo iliyoandaliwa na Tume inayoongozwa na jaji Warioba.

Wananchi wakifuatilia kwa makini maoni mbalimbali

Baadhi ya wananchi wakinyoosha mikono kuashiria kukubaliana na maoni ya mwenzao aliyependekeza vyeo vya ukuu wa wilaya na mkoa kuondolewa kabisa kwenye katiba mpya na badala yake viongozi wa ngazi hizo wachaguliwe na wananchi wa maeneo husika. Zoezi hilo la kutoa maoni lilikuwa linasimamiwa na Dk Slaa

Wanasheria vijana wakiwafafanulia wananchi vipengele mbalimbali vya rasimu ya Katiba. Mwenye suti ni James Lyatuu na mwenye tisheti ya mistari ni Mathias Lyamunda

Kulikuwa na fomu nyingi zilizogawiwa kwa wananchi wengine kutoa maoni yao kwa kuandika kama huyu

Wakili Marando akisoma habari kwenye gazeti

Dk Slaa akibadilishana taarifa na viongozi wa Mkoa wa Arusha na Kanda ya Kaskazini, wakati huo huo Marando akizungumza na Ally Bananga

Kamanda Waitara akibadilishana mawazo na makamanda wa Arusha wa Chadema, Ally Bananga, Haleluya na

Viongozi wote na wananchi walikaa kimya kwa muda wa dakika moja kama ishara ya kumbukumbu za wananchi waliouwawa kwa kulipukiwa na mabomu katika mkutano wa chadema jijini Arusha kwenye uwanja wa Soweto Juni 15, 2013.

DSC08708

Mzee OleKisambo, ambaye aliwahi kugombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mgaharibi akitoa maoni yake kwa Dk Slaa.

DSC08711

Walemavu pia walipata nafasi kuwasilisha maoni yao…

Mmoja wa kina dada waliojitokeza kuto amaoni yao pia

Jukwaa kuu nao walipata fursan ya kutoa maoni yao kwa kujaza fomu maalumu

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kutoa maoni yao kuhusiana na rasimu ya Katiba Mpya

PICHA ZOTE NA SERIAJr

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO