Taarifa ambazo Blog hii imezipata muda huu kutoka Tabora zinaeleza kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imetoa maamuzi yake juu ya shauri la kesi ya ugaidi kwa washtakiwa, Henry John Kileo, Evodius Justian, Oscar Kaijage, Seif Kabuta na Rajab Kihawa kwa KUFUTA MASHTAKA YA UGAIDI dhidi yao.
Mke wa Katibu wa Chadema Kanda Maalumu ya dar es Salaam Henry Kilewo; Bi Joyce Kiria akiwa ndani ya chumba cha Mahakama kabla ya hukumu kutolewa
Picha ya Maktaba, watuhumiwa waliofutiwa mashitaka ambayo Chadema walieleza mkakati wake kabla hata hayatekelezwa
Henry Kilewo mwishoni ukutani akiwa na fikra nzito labda kwa kutokujua hatma ya hukumu dhidi yake na wenzake mapema leo
Mke wa Henry Kilewo, Bi Joyce Kiria akiwa na tabasamu pana
PICHA ZOTE KWA HISANI YA JOYCE KIRIA
Jikumbushe
Maamuzi haya yanafuatia kesi hiyo ya rufaa ya jinai namba 53/2012 ilifunguliwa na Wakili wa Utetezi, Peter Kibatala na kuanza kusikilizwa Julai 22 mwaka huu mbele ya Jaji Lukelelwa ikiomba miongozo ya kisheria ikiwemo yaliyotolewa na mahakama za wilaya na mkoa.
Shauri la maombi ya marejeo liliwakilishwa na Wakili Peter Kibatala anayewatetea washitakiwa, akiiomba mahakama kuu ipitie majalada ya kesi mbili dhidi ya wateja wake zilizofunguliwa mahakama hizo baada ya kuona maamuzi yake hayakutenda haki.
Wakili Kibatala alibainisha katika maombi hayo kwamba kutokana na maamuzi hayo ya mahakama za chini yameathiri pia haki za waomba rufaa ikiwa ni pamoja na kuwanyima haki ya kupata dhamana.
Kwa upande wake Serikali ilishindwa kujibu maombi hayo, badala yake ilijenga hoja kwamba walichelewa kupata nyaraka hizo kwani walizipokea siku moja kabla ya kutajwa shauri hilo hivyo walishinda kuzijibu.
0 maoni:
Post a Comment