Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

News Alert: Tindu Lissu aibuka kidedea katika kesi ya kupinga Ubunge wake.

Lissu Mahakama Kuu imemuachia Mh Tindu Lissu kuendelea na ubunge wake (Singida Mashariki) baada ya hoja za walalamikaji kushindwa kuthibitisha madai yao.

Habari zaidi zinaeleza kuwa…

  • Hoja zote za upande wa mlalamikaji zatupwa.
  • Maofisa Jeshi pamoja na kikosi maalum wahudhuria mahakamani.

Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu, ameshinda kesi iliyofunguliwa dhidi yake mjini Singida kupinga ushindi uliomweka madarakani

Hukumu imetolewa na Jaji Moses Mzuna anayetoka Mahakama Kuu kanda ya Kilimanjaro, iliyofunguliwa na makada wawili wa CCM, Shabani Itambu na Pascal Hallu.

Leo mahakamani wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa, wananchi wa Singida, na waandishi wa habari walijitokeza kwa wingi sana katika eneo la mahakama.

Idadi ya Polisi pia ilikuwa kubwa, ndani na nje ya Mahakama. Kilicho kuwa cha ajabu kidogo leo getini maofisa wote wakubwa wa Jeshi la Polisi walikuwepo pale na kikosi maalumu kwa ajili ya kukagua kila anayeingia Mahakamani,  kila mtu aliyekuwa anaingia mahakamani alipekuliwa hadi wabunge waliokuja kusikiliza kesi hiyo.

Akisoma hukumu Jaji Moses Mzuna alisema “HOJA YA TISA, Kama Mgombea wa walalamikaji (CCM) alikataa kusaini matokeo. Hoja hii haipaswi kunipotezea muda sana. Njau hakuhudhuria, aliwakilishwa na mlalamikaji wa kwanza ambaye alikataa kusaini matokeo.

Wakili wa serikali alisema, kukataa pekee kusaini matokeo hakusaidii kutengua matokeo. Hivyo hata hoja ya tisa naitupilia mbali. Haikuwa sahihi.

Hoja ilitolewa hapa, kuwa mawakala walikula kiapo kwa hakimu. Walalamikaji walisema kuwa walipaswa kula kiapo kwa msimamizi wa uchaguzi. Je kuapishwa na hakimu kunabatilisha matokeo?

Hoja zilizotolewa na mawakili wa Serikali walisema Hakimu ana mamlaka ya kutoa viapo. Binafsi nasema kuwa waliotunga sheria hawakumaanisha kuwa Mahakimu hawaruhusiwi kuapisha mawakala, vinginevyo kungekuwepo Fomu ya hakimu tu. Lakini fomu zinaonyesha hakimu, Msimamizi wa uchaguzi na Msimamizi msaidizi, fomu inatambulika kisheria, kwa sheria ya Uchaguzi. Hii haihusiani na zoezi la uchaguzi.

Katika kesi ya Prince Bagenda Vs Wilson masilingi, katika kesi hii mawakala walifanya kazi bila kuapishwa, na ilichukuliwa kuwa sehemu ya kutengua uchaguzi, angalia pg 240.

Kwa lugha yake Jaji alisema hawakuwa na mamlaka halali, lawful mandate, lakini ilisaidia kutengua, na mwanasheria wa serikali alihusika katika hili.

Maelezo hayo yanatofautiana na kesi iliyo mbele yangu, jimbo la Singida Mashariki mawakala walikula kiapo, na walikuwa na mamlaka halali. Hivyo hoja hii naitupilia mbali

HIVYO, UCHAGUZI ULIKUWA WA HAKI, NA TUNDU LISSU NI MBUNGE HALALI NA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA WA HAKI, HIVYO SIWEZI KUTENGUA.

Walalamikaji wa kesi hiyo, iliyofunguliwa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma, walikuwa wanatetewa na wakili Godfrey Wasonga, kutoka mkoani Dodoma, huku Lissu akijisimamia mwenyewe.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Machi 12, 2012, kufuatia makada wawili wa CCM, kupinga ushindi wa Lissu kwa madai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na dosari nyingi.

Awali Katika mahojiano na Lissu, alisema vyovyote mahakama itakavyo hukumu, anajivunia kuimarisha demokrasia na kuwa Mbunge wa kwanza kutoka upinzani, kwenye historia ya mikoa ya kanda ya kati.

Maelezo na LUKAZA BLOG kwa Hisani ya Media 2 Solution Blog!

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 maoni:

SeriaJr said...

Haki ziku zote haipotei... Mungu ataendelea kuwapigania wote waliosimama katika haki!

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO