Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Samatta ampa ulaji Kaseja huko Kongo

*Atengewa dau la mil 50 Kongo

*Mwenyewe asema yupo tayari kujiunga nao

MFANO mzuri unaooneshwa na wachezaji wa Tanzania, wanaocheza soka la kulipwa nchini Kongo DRC, katika klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu umewavutia klabu ya FC Lupopo ya nchini humo, ambao wamekuja kuteta na aliyekuwa kipa wa Simba, Juma Kaseja ili kujiunga na timu yao.

Kaseja ambaye ni golikipa namba moja wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, ametengewa kiasi cha Dola za Kimarekani 30,000 ambazo ni Shilingi milioni 50 za Kitanzania iwapo atakubali kujiunga na timu hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa timu hiyo, Balanga Ismail alisema wanamuhitaji mchezaji huyo, ndio maana wameamua kutua nchini kufanya naye mazungumzo.

“Kaseja ni kipa mzuri na tunamfahamu kwa muda mrefu, pia tunawapenda wachezaji wa Kitanzania, hasa kutokana na mfano mzuri anaouonyesha Mbwana Samatta, akiwa na klabu ya TP Mazembe nchini kwetu.

“Tumemwekea dau zuri mezani ili kumsajili, kwa kuwa alikuwa kipa namba moja, tunaamini atatua kwetu, ikizingatiwa ni mchezaji huru hivi sasa,” alisema Ismail.

Naye, Kaseja alisema ameshaanza mazungumzo rasmi ya awali na klabu hiyo, na endapo watafikia muafaka basi atasaini nao mkataba wa kuichezea timu hiyo.

“Lupopo wameonesha nia ya kunisajili na nimeanza rasmi mazungumzo nao, kikubwa nitaangalia maslahi kwa kuwa hii ndiyo kazi yangu, ambayo pia inaniongoza katika maisha,” alisema.

Endapo Lupopo watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo, basi atakuwa mchezaji wa nne wa Kitanzania, kuchezea klabu kubwa za Kongo, kwani mbali na Samatta na Ulimwengu, timu ya FC Motemapembe iliwahi kumsajili, Mussa Mgosi kutoka Simba, ambapo hivi sasa imemtema mchezaji huyo.

Chanzo: Mtanzania

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO