Tunakusogezea karibu habari na matukio, zaidi habari za kisiasa na utawala, matukio ya Arusha na maeneo jirani, bila kusahau na mambo mengineyo ya kitaifa yanayojiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu maendeleo na kuwa ya maslahi kwa watu wengi. Burudani na michezo pia havijasahaulika. Kizuri zaidi, unaweza kupata link ya Blogu nyingine na website muhimu hapa hapa kwa kuscroll mpaka chini. Karibu tuhabarike!

Bloga wa Arusha Wakutana Kuanzisha Umoja wao

Ikiwa teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya mtandano inazidi kukua na kupata umaarufu miongoni wa watanzania, wadau wa uliongo huo kwa Mkoa wa Arusha wameamua kuanzisha umoja wao ambao utalenga kuwatambulisha mbele ya jamii na mamlaka za nchi sambamba na kuongezeana ujuzi katika kuiboresha zaidi.

Mkoa wa Dar es Salaam unaonekana kuwa na wadau wengi zaidi. Mikoa mingine wapo pia, ikiwamo Arusha lakini hawafahamiki sana kitaifa kama ilivyo maeneo mengine. Kwa kutambulika na mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, teknolojia hii inapaswa kuenziwa na kusimamiwa vyema ili jamii iweze kunufaika nayo vizuri, na wahusika nao wakinufaika kwa namna moja au nyingine.

Teknolojia hii katika uwanja wa mawasiliano inahusisha pia mitandao mingine ya kijamii kama Facebook, Tweeter n.k bila kusahahu wavuti za makampuni ama watu binafsi.

Baadhi ya maBlogga wa Jijini Arusha waliokutana katika kikao cha kujadili mustakabali wa ushiriki wao katika dunia ya utandawazi hasa katika matumizi ya mitandao ya kijamii, lengo la kukutana kwao ikiwa ni kupanga mikakati ya kuanzisha umoja wa blogga wote wanaoishi ama kufanya shughuli zao Jijini hapa.

Kutoka kushoto, majina yao na anuani za blog kwenye mabano ni Woinde Shizza kutoka LIBENEKE LA KASKAZINI (http://woindeshizza.blogspot.com; Thomas wa JITAMBUE KWANZA BLOG (http://jitambuekwanza.blogspot.com/); Gadiola Emmanuel wa WAZALENDO25 (http://wazalendo25.blogspot.com/); (Victor Machota wa ASILI YETU TANZANIA (http://victormachota.blogspot.com) na Bertha Mollel wa BERTHA BLOG (http://berthamollel.blogspot.com/). Bloga mwingine ambaye haonekani pichanni ni Seria Tumainiel wa NOISE OF SILENCE (http://arusha255.blogspot.com)

SeriaJr wa Arusha255 (mwenye sweta) akifurahia jambo na wajumbe wengine

Umakini katika kusikiliza mjadala na maoni ya wengine

Bertha Mollel na Victor Machota wakibadilishana mawazo baada ya kikao kumalizika

Woinde Shizza na Gadiola Emmanuel na mapoooz. Wadau hawa waliokutana ni sehemu ndogo tu ya Bloga wa Arusha ambao hawakuweza kuhudhuria.

Washirikishe Google Plus

About SeriaJr

SeriaJr will keep you updated with all current political news countrywide "Ndiye "Bosi" Mzito Arusha255" Karibu Tuhabarike!.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

TANZANIA, THE HOME OF KILIMANJARO