Miji ya Arusha na Moshi imezizima kwa simanzi tena baada ya kutokea kwa kifo cha mfanyabiashara wa madini Mererani aliyeuwawa kwa kupigwa risasi mchana wa leo. Mfanyabiashara huyo maarufu kama Erasto amefikwa na mauti baada ya kushambuliwa na kinachodhaniwa kuwa risasi za moto maeneo ya Mijohoroni jirani na Kia Wilayani Hai.
Pichani juu baadhi ya wananchi na askari wakiushangaa mwili wa marehemu
Itakumbukwa kwamba ni takribani wiki moja tu imepita tangia mfanyabiashara mwingine Onesmo Lyimo kuuwawa kwa risasi akiwa ndani ya shimo Mirerani. Julai 20, 2013. Mtuhumiwa naedaiwa kuhusika na kifo cha Onesmo ametambulishwa kwa jina la utani kama Chusa.
Pia redio za Arusha hapa ziliripoti tukio jingine lililotokea alfajiri ya jana likimhusisha mfanyabaiashara mwingine (jina linahifadhiwa) aliyedaiwa kulawitiwa na watu wasiojulikana lakini ikiaminika wakiwa wamekodiwa kufanya ukatili huo.
Gari iliyoubeba mwili wa marehemu na kuupeleka mochwari
Baadhi ya majeraha aliyokutwa nayo marehemu mara baada ya kufikishwa mochwari. Kwa mujibu wa taarifa zilizozagaa eneo la tukio na kutoka kwa marafiki wa marehemu (bado hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi) zinaeleza kwamba marehemu Erasto ambaye ana biashara kadhaa katika Jiji la Arusha ikiwemo SG Resort, hoteli anayoimiliki, aliitwa na watu waliodai kutaka kumuuzia madini. Alipofika eneo hilo na kuanza kufanya biashara, ndipo akashambuliwa ghafla na watu hao kutoweka.
Gari inayosadikiwa kutumiwa na marehemu
RIP ERASTO!
0 maoni:
Post a Comment