Vyama viwili vya kisiasa nchini Zimbabwe vimemuunga mkono waziri mkuu Morgan Tsvangirai katika uchaguzi ujao wa urais.Vyama hivyo vimeahidi kuunda serikali ya umoja baada ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 31.
Jumapili, waziri wa fedha wa zamani na mshirika wa karibu wa zamani wa rais Robert Mugabe, Simba Makoni alisema kuwa ameunda ‘ chama mseto cha mabadiliko' na waziri mkuu Morgan Tsvangirai na chama kingine cha kisiasa kwa lengo la kumshinda bw. Mugabe katika uchaguzi wa Julai 31.
Uamuzi wa vyama hivyo vya kisiasa kuunda ushirika huenda ulitokana na somo walilolipata kufuatia uchaguzi wa 2008 ambapo bw.Tsvangirai alishindwa kupata wingi wa kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi. Katika uchaguzi huo bw. Makoni alipata asili mia 9 ya kura.
Jumapili, bw. Tsvangirai alisema atagombania urais Julai 31 licha ya kutoridhishwa na ukosefu wa mabadiliko ya kidemokrasia katika taifa hilo. Lakini wizara ya fedha ya Zimbabwe inasema itahitaji takriban dola milioni 132 kugharamia uchaguzi huo.
Waziri wa fedha bw. Tendai Biti anasema itambidi bw. Mugabe kuyasukuma makampuni ya migodi ya almasi kutoa fedha za mauzo ya madini hayo iwapo uchaguzi huo utaendelea. Uhcaguzi huo utaashiria kumalizika kwa serikali ya muungano baina ya bw. Mugabe na bw. Tsvangirai iliyoundwa baada ya uchaguzi wenye utata wa 2008.
Chanzo: Reuters
0 maoni:
Post a Comment